30.8 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

WAKAZI MABONDENI DAR CHUPU CHUPU KUZAMA

yake baada ya maji kujaa kutokana na mvua iliyonyesha jana

Na ASHA BANI,

WAKAZI wa Mabondeni jijini Dar es Salaam jana walinusurika kukumbwa na mafuriko baada ya maji kujaa katika Mto Msimabazi kutokana zilizonyesha kwa wingi maeneo ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.

Katika Jiji la Dar es Salaam mvua zilizonyesha kwa wastani lakini katika hali ya kushangaza nusura zisababishe maafa katika maeneo ya Jangwani, Kigogo na maeneo yanayozunguka Mto Msimbazi.

Katika maeneo ya Buguruni, Bonde la Magomeni Mikumi na Buguruni kwa Mnyamani nyumba zikiwa zimejaa maji na wananchi wakionekana kuomba msaada wa kuokolewa.

Eneo la Jangwani ni lile ambalo serikali ilishawahi kupiga marufuku wakazi hao kuendelea kuishi lakini baada ya msimu wa mvua kwisha wameonekana kurudi tena kama zamani.

Mkazi Mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Issa alisema serikali inatakiwa kuwatilia mkazo na kuwaondoa tena kwa nguvu ili kuzuia maafa zaidi yanayoweza kujitokeza.

Baadhi ya wapiti njia kando kando ya Bonde la Jangwani walionekana kuwashangaa wananchi hao kugoma  kuondoka tangu wakati Mkoa huo ukiwa chini ya Said Meck Sadick.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles