25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Wakazi kuwasaidia wasanii wakike

Jeremia Ernest, Zanzibar.

NYOTA wa muziki wa hip pop nchini, WabiroWassiramaarufu kwa jina la Wakazi, ameweka wazi mipango yake ya kutaka kuwasaidia wasanii wa kike kufikia ndoto zao.

Wakazi ni miongoni mwa wasanii ambao wametoa shoo kali katika tamasha la Sauti za Busara msimu wa 17 ambalo limemalizika jana katika eneo la kihistoria Ngome Kongwe, Zanzibar.

Akizungumza na MTANZANIA baada ya kushuka kwenye jukwaa hilo alisema amejikita kufanya kazi na wasanii wakike katika bendi yake kwa kuwa anatazamia kusimamia ndoto zao katika muziki.

“Wasanii wa kike wanapata changamoto nyingi wakiwa katika safari ya kutoka kimuziki nimeamua kuwashika mkono ili kuleta mabadiliko katika tasnia yetu, nina wasanii wa kike tu katika bendi yangu” alisema Wakazi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles