Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameendelea kutoa maoni juu ya Tozo za Miamala ya Simu na Benki kufuatia ufafanuzi wa Serikali uliotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, pamoja na Mawaziri wengine
Wakizungumza na Mtanzania Digital kwa nyakati tofauti wengi wa wakazi hao wameeleza kuwa, hawakuwa wakijua kinagaubaga Tozo hizi zinatumikaje lakini baada ya Ufafanuzi uliotolewa, wako tayari kulipa Tozo kama mchango wao katika maendeleo ya Taifa letu
Aidha, wakazi hao wa Jiji la Dar es Salaam, wametoa wito kwa Wananchi wengine kulipa Tozo kwani Serikali inategemea Tozo hizo katika kuliletea Taifa maendeleo, na kama tutakuwa waziro katika ulipaji wa Tozo tutakuwa tunachelewesha maendeleo yetu wenyewe.
“Tozo ni muhimu katika kuchochea maendeleo na kuboresha huduma za kijamii, tuko tayari kulipa tozo na tunatambua umuhimu wake katika maendeleo ya taifa letu, katika hili tyunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan.
“Tunaona faida zake ikiwamo vituo vya afya, barabara na huduma nyingine kama sababu zinazotupa msukumo wa kuchangia kidogo kupitia tozo zilizowekwa na Serikali yetu ili kuharakisha upatikanaji wa huduma hizo kote nchini,” wameeleza wakazi hao.