24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi 500,000 Mto Msimbazi kulipwa fidia

Na John Dande

-Dar es Salaam 

WAKAZI zaidi ya 500,000 wanatarajia kulipwa fidia kupisha mradi wa ujenzi wa Mto Msimbazi ili kuepusha madhara yanayotokea wakati wa mvua.

Akizungumza mjini hapa jana wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua madhara yanayotokea kwa wanaoishi pembezoni mwa mto huo pindi mvua zinaponyesha, Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CCM), alisema endapo mradi huo utafanikiwa utakuwa ni suluhisho la kudumu kwa wakazi hao.

“Wizara ya Tamisemi tayari wameshatafuta suluhisho la kudumu ikiwa ni kuomba mkopo wenye masharti nafuu kwa Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya kulipa fidia,” alisema Mtulia.

Alisema tayari WB imekubali na kinachosubiriwa ni Wizara ya Fedha na Mipango kuidhinisha.

 “Benki ya Dunia wamekubali kutoa fedha kiasi cha dola milioni 100 na kinachosubiriwa ni Wizara ya Fedha kuidhinisha,” alisema Mtulia.

Pia alisema mradi huo wa kudumu ukifanikiwa katika bonde hilo kutakuwa ni sehemu nzuri ya kupumzikia.

Naye mkazi wa Kigogo, Ramadhani Yahaya, alisema mvua zimekuwa zikileta madhara makubwa ikiwamo kukosa sehemu ya kuishi.

“Mvua zimekuwa zikituathiri, mwaka 2011 wakati wa mvua nyumba saba ziliondoka na maji na kwa sasa zinaponyesha tunalazimika kuhama makazi,” alisema Yahaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles