27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Wakamatwa wakiwauzia wanafunzi mirungi

mirungiNa UPENDO MOSHA, MOSHI

WALIMU wa Shule ya Sekondari Scolastika iliyoko Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro, wamewakamata vijana wawili, wakazi wa mji mdogo wa Himo, wilayani hapa wakituhumiwa kuwauzia wanafunzi wa shule hiyo dawa za kulevya aina ya mirungi.

Mkuu wa Shule hiyo, Michael Shiloli, aliliambia MTANZANIA, kwamba vijana hao walikamatwa juzi na walimu waliokuwa wakikagua usalama wa shule kwa kushirikiana na baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa Mwalimu Shiloli, vijana hao walikamatwa wakiwa na dawa hizo, sigara, chipsi na biskuti.
“Walikuwa wamevifunga katika boksi kwa lengo la kuwauzia wanafunzi wa shule yetu, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Wakati walimu wakiwa kwenye doria, waliona bodaboda ikipita kando ya uzio wa ukuta na kumwona dereva wake akirusha kamba kwa juu.

“Kamba hiyo ilipokelewa na mwanafunzi kwa chini ikiwa imefungashwa boksi lenye mirungi, sigara, chips na biskuti.

“Baada ya walimu hao kushuhudia tukio hilo, walilazimika kuwakamata vijana hao wawili ambao ni mwendesha bodaboda aitwaye Musa Omari na Amiri Abdalah.

“Baadaye, waendesha bodaboda wapatao 15 hivi, waliwavamia walimu lakini polisi waliwahi na kuwatawanya,” alisema mwalimu huyo.

Naye  Mwalimu wa Nidhamu wa shule hiyo, Laban Elima, alisema mmoja wa wanafunzi waliokuwa wakipokea boksi hilo alikutwa amevaa saa yenye simu waliyokuwa wakiitumia kuwasiliana na watuhumiwa hao.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbod Mutafungwa, alithibitisha kukamatwa kwa vijana hao.

“Kwa  kuwa imebainika mwenye chipsi hizo ni Amiri Abdalah na ndiye mwenye mzigo uliokamatwa ikiwemo mirungi, lazima uchunguzi wa kina ufanyike na asiachiwe kiholela,” alisema Kamanda Mutafungwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles