29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

WAKAMATWA WAKIIBA MAFUTA YA UJENZI STANDARD GAUGE

Na Lilian Justice, Morogoro


JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro  limewakamata watuhumiwa tisa  wakidaiwa kuiba    dizeli lita 570  mali ya kampuni  zinazojenga reli  ya mwendokasi (Standard  Gauge),  maeneo ya Ngerengere wilayani Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa, alisema  tukio hilo lilitokea   Julai 7 mwaka huu   jioni.

Alisema kutokana na  msako mkali wanaouendesha waliweza kuwakamata vijana tisa wakiwa na    dizeli lita 570 yakiwa kwenye madumu ya lita 20  na lita 40 .

Kamanda  alisema   mafuta hayo ni mali ya kampuni  zinazojishughulika na  ujenzi wa reli   ya mwendo kasi  zilizopo Ngerengere.

Alisema     watuhumiwa wanaendelea kushikiliwa  na  jeshi hilo litaendelea kuwabaini wote wanaohujumu  ujenzi wa taifa.

Katika msako huo, polisipia  walikamata dawa za kulevya zinazodaiwa ni heroine  kete 47  na bangi puli 15 na misokoto 160.

Alisema tukio hilo lilitokea Julai 30   mchana   maeneo ya Manzese  manispaa ya Morogoro  ambako Anna Selestine (30) alikamatwa na  madawa  hayo akiwa ameyahifadhi katika   kikopo cheusi.

Kamanda   alisema    uchunguzi unaendelea  na hatua za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa zinaendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,587FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles