24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAKALA WAHAKIKI MIZANI 1,500 ZA KUNUNULIA PAMBA

 

 

Na Derick Milton,

WAKALA wa Vipimo Tanzania  (WMA) imeendelea na uhakiki wa mizani kwa makampuni ya kununua  pamba mkoani Simiyu katika kuhakikisha wakulima wa zao hilo hawaibiwi.

Vilevile imekagua mizani za wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa mazao ya nafaka na kutoa elimu.

Meneja wa WMA mkoani Simiyu, Augustine Maziku, alisema mizani 1,500 tayari imekaguliwa kutoka makampuni hayo na wafanyabishara.

Maziku alisema hatua hiyo ya kutoa elimu  na uhakiki wa mizani inayotumika kununulia pamba na mazao mbalimbali linaendelea kwa  kwa wananchi wote ambao wana maduka ya kuuza nafaka.

Alisema wakala inatarajia kutembelea vijiji vyote mkoani humo kutoa elimu na kufanya ukaguzi wa kushtukiza kwa wanunuzi wa pamba.

Hatua hiyo ina lengo la  kuona kama mizani iliyopimwa na ikaonekana ni sahihi inaendelea kununua pamba ya wakulima kwa vipimo sahihi.

“Kuna wakulima wanalalamikiwa kuweka maji, kokoto  na mchanga kwenye pamba kwa ajili ya kuongeza uzito.

“Tunawataka waache tabia hiyo mara moja, sheria ya vipimo ipo na inafanya kazi kwa pande zote mbili muuzaji na mnunuzi, wote kwa pamoja hawatakiwi kufanya udanganyifu wowote katika biashara,” alisema Maziku.

Meneja  wa WMA makao makuu, Richard Kadege alisema lengo kuu  la kukagua mizani na kutoa elimu kwa ajili ya kumlinda mlaji.

Alisema hatua hiyo itamwezesha mlaji  apate faida na thamani ya kile alichozalisha  na siyo kupunjwa na wafanyabiashara  wajanjawajanja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles