23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wajasiriamali Wanawake 700 Songea wamenufaika na mikopo ya riba nafuu ya TPB

Waziri wa Nchi Sera Mbunge Ajira vijana na walemavu, katika Ofi si ya WaziriMkuu, Jenista Mhagama (kulia) akikabithi mfano wa hundi yenye thamani ya Milioni 389.2/= iliyotolewa na Benki ya Posta kwenye kikundi cha Vicoba kilichopo Songea mkoani Ruvuma ambacho kipo chini ya mwavuli wa shirika la masista wa Imakulata DMI.
Waziri wa Nchi Sera Mbunge Ajira vijana na walemavu, katika Ofi si ya WaziriMkuu, Jenista Mhagama (kulia) akikabithi mfano wa hundi yenye thamani ya Milioni 389.2/= iliyotolewa na Benki ya Posta kwenye kikundi cha Vicoba kilichopo Songea mkoani Ruvuma ambacho kipo chini ya mwavuli wa shirika la masista wa Imakulata DMI.

Na Harrieth Mandari,

Wajasiriamali zaidi ya mia saba wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamenufaika na mikopo yenye masharti na riba nafuu inayotolewa na Benki ya Posta nchini (TPB) kwa ushirikiano na Baraza la Taifa Uwezeshaji Uchumi (NEEC) kwa wananchi kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mikopo hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 542 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu Bunge, Ajira kwa Vijana na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma, alitumia fursa hiyo kutoa maagizo kwa watendaji wa mkoa huo kusimamia uanzishwaji na uboreshwaji wa vyama vya akiba na mikopo.

Alisema njia pekee ya kuwakwamua wananchi kiuchumi  wenye kipato kidogo ni kuwasaidia elimu ya uanzishaji vikundi vya ujasiriamali na kuwatafutia fursa ya kuweza kupata mikopo yenye riba na masharti nafuu.

Akaongeza kuwa hilo ni jukumu la Serikali ambapo moja ya kipimo kwa Maafisa Maendeleo ya jamii katika Utendaji kazi ni pamoja na utekelezaji wa kuwepo kwa vyama vya akiba na mikopo vya wanawake na vijana.

Aidha aliwataka wanufaika wa mikopo hiyo ambao ni wanawake na vijana waliokopeshwa pikipiki kwa ajili ya biashara,  kutumia fedha hizo kwa malengo waliyoyakusudia badala ya kuitumia mikopo kinyume na malengo na taratibu za benki.

Mkopo huo uliotolewa kwa wajasiriamali waliojiunga kwenye vikundi vya akiba na mikopo pamoja na vikundi vilivyoko chini ya shirika la masista wa kanisa katoliki la DMI ni moja ya utekelezaji na uboreshaji wa huduma za TPB kwa wananchi wa kipato cha chini ili waweze kujikwamua iuchumi.

Naye Afisa Mtendaji Mkuuwa TPB,  Sabasaba Moshingi alisema lengo la Benki hiyo ni kutoa mikopo kwa vikundi mbalimbali vya wafanyabiashara na wajasiriamali ni kupiga vita umaskini kwa kuwaelimisha na kuhamasisha wananchi wa kawaida kuzitumia huduma hizo zenye gharama na masharti nafuu.

Alisema kwa kushirikiana na NEEC wameanzisha utoaji wa mikopo nafuu kwa wajasiriamali na baraza limekuwa likisimama kama mdhamini wa mikopo hiyo na kuwa wanawake wameonesha kuwa  waaminifu kwenye huduma za mikopo pamoja na majukumu ya kijamii yanayowakabili.

Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa Uwezeshaji Uchumi Beng’i Issa ambayo imejikita zaidi katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kupiga vita umaskini limekuwa likiwadhamini wajasiriamali wanaokopa kwenye Benki hiyo ya Posta huku alisema kipaumbele cha baraza hilo kwenye udhamini kimeelekezwa zaidi kwa wanawake kwa sababu ya umuhimu wao katika jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles