25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wajarisiriamali wanahitaji mikopo ya mali na vitendea kazi

Amani Mkokote
Amani Mkokote

Na YASSIN ISSAH, DAR ES SALAAM

Licha ya kuwa safari ya maisha ili kuweza kufika malengo inapitia katika hatua ndefu ikiwa kuna wanaokwama na kuamua kukata tamaa kabisa kuweza kuendelea mbele lakini kinachotakiwa ni mtu mwenyewe kuamua na kujizatiti katika kuhakikisha anapambana ili aweze kujikwamua kuwa na maisha mazuri.

Hakuna kibonde katika maisha kwani maisha ni mapambano.

Suala la kujituma kwa kuamua kupangilia baadhi ya mambo kwa kupitia njia ambazo ni halali zisizoweza kuhatarisha maisha ya mhusika mwenyewe ikiwa ni kwa kujishughulisha na kazi ili mradi kuweza kupata riziki ya kuendeshea maisha ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuhudumia familia husika.

Hii hasa huhusan kwa vijana ambao wamekuwa wakichagua kazi, wengi wao wamekuwa wakitaka kazi za kukaa ofisini tu na sio nyingine za ujasiriamali ambazo zitaweza kuwasaidia kuweza kufika malengo yao hata kwa kuanzia na kipato kidogo kwani siku zote mwanzo mgumu.

Bila kuitegemea Serikali itoe ajira, tunaweza kuijikita katika baadhi ya kazi ndogondogo na kujiajiri wenyewe kwenye kazi za kutumia nguvu na zisizotaka mtaji mkubwa ili kupata kipato katika nyanja mbalimbali ikiwamo uchomeleaji wa vyuma, ususi, ufugaji wa kuku, ufundi seremala, utengenezaji wa mapambo ya ndani ya aina tofauti tofauti, uchongaji wa vinyago au hata bustani za miti na maua.

Kijana Amani Mkokote ni fundi wa kushona nguo ili kujipatia fedha za kuendeshea maisha yake, alipotembelewa na MTANZANIA na kutanabah ifuatavyo:

MTANZANIA: Nini kilifanya uwe fundi wa kushona nguo?

AMANI: Kushona nguo ni fani ambayo nilikua naipenda toka zamani kama zilivyokazi nyingine ambazo watu wanafanya ili kuwaingizia kipato, ndiyo sababu kubwa iliyonifanya nipende kuwa fundi wa kushona nguo.

MTANZANIA:Una muda gani unafanya kazi hii?

AMANI:Nina muda wa miaka 20 nipo kwenye kazi hii ya kushona na safari yangu ya ufundi ilianzia nikiwa Songea baadae nikahamia mkoani Iringa wilaya ya Makete, halafu nikahamia katika jiji la Mbeya na mwishao nikaja Dar es Salaam.

MTANZANIA: Nini kilikufanya uhame mikoani na kuja Dar?

AMANI: Ni kutokana na mzunguko wa uchumi na biashara kwa ujumla kutokana na hali ya kwamba mikoani kazi zinakuwepo lakini  za msimu na kipato kidogo, tofauti na huku Dar, ambako kazi zinakuwa nyingi na kipato chake kinakuwa kingi vilevile. Aghalabu kutokana na wingi wa watu na asilimia kubwa ya watu hao wanapenda wapendeze ili wawe na mwonekano mzuri kutokana na ushindani wa maisha.

MTANZANIA:Umepata mafanikio yapi mpaka sasa kupitia kazi hii?

AMANI:Nimefanikiwa kufungua ofisi yangu maeneo ya Tabata Segerea ingawa bado naendelea kujituma zaidi ili niweze kusonga mbele zaidi maana kazi hii ndio inayoniwezesha kumudu familia yangu na kutimiza majukumu mengine ya maisha.

MTANZANIA: Changamoto zipi unakutana nazo katika kazi hii?

AMANI:Changamoto ninayoipata ni kukosa mataji wa kuendeleza biashara hii unakuwa ni tatizo ikiwa tunajaribu kuomba mikopo kwenye mabenki tunapewa pesa ndogo isiyoweza kukidhi mahitaji, unaomba mkopo wa shilingi milioni moja lakini unapewa shilingi laki mbili ambazo haziwezi kununua bidhaa za kutosha na wenye mali hawakopeshi. Hivyo tunashindwa kufikia malengo.

MTANZANIA: Unazikabili vipi changamoto hizo?

AMANI: Ninachokifanya ni kuweza kufanya kazi kwa kujituma zaidi ili nihakikishe kuwepo sokoni na wateja wangu siwapotezi  kwani nikiwapoteza wateja kazi hazitoweza kufanyika. Kwani wateja wakihamia sehemu nyingine  ngumu kuwarudisha na vilevile ninaimarisha  uaminifu kwani mafundi washoni wengi tumekuwa na changamoto ya kutomaliza kazi za wateja wetu kwa wakati sahihi.

MTANZANIA: Malengo yako ni yapi zaidi?

AMANI: Ninahitaji kujikita zaidi kwa kufanya kazi zaidi ili niwe mbunifu wa mavazi ya aina mbalimbali kama ilivyo kwa wabunifu wengine ambao naona kazi zao  jinsi zilivyo nzuri na wameweza kufika mbali kupitia kazi hii hivyo naamini na mimi nitafanikiwa pia kwa kujituma zaidi kupitia kazi hii ya ushonaji.

[email protected] / 0714325980

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles