23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wajane wamlilia Magufuli kunyang’anywa mashamba

 DERICK MILTON – TARIME

WAJANE sita katika Kijiji cha Sombanyasoko, Kata ya Komaswa, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, wamemwomba Rais Dk. John Magufuli awasaidie ili waweze kurudishiwa mashamba yao zaidi ya ekari 80 ambazo wamedai wamenyang’anywa na mmoja wa wanakijiji.

Walidai kuwa wamenyang’anywa maeneo yao ambayo waliachiwa na waume zao kabla ya kufariki, na wamehangaika kutafuta haki hadi mahakamani, lakini wameshindwa kwa kile walichodai uwepo wa vitendo vya rushwa katika kesi yao.

Mbali na wajane hao, katika mgogoro huo wa ardhi ambao umedumu kwa muda wa miaka saba, zipo familia nyingine nne kwenye ekari hizo 80 ambazo nazo zimemwomba Rais Magufuli kuwasaidia wapate haki yao.

Mmoja wa wajane hao, Mang’era Nyaswi alisema kuwa wamenyang’anywa mashamba yao baada ya kuingizwa katika mgogoro wa ardhi ekari sita za watu watatu ambao walikuwa wanashtakiana katika baraza la ardhi la kata.

Mang’era aliwataka wananchi hao kuwa ni Daniel Chacha na Meng’anya Magoti waliokuwa wanashtakiwa na Mseti Gachuma kwa madai ya kumiliki ardhi ekari sita ambayo siyo mali yao.

Alisema kuwa katika kesi hiyo Gachuma alishindwa baada ya hukumu ya baraza hilo kutoa haki kwa washtakiwa, na baaada ya hukumu hiyo alikata rufaa Baraza la Ardhi Wilaya Tarime.

“Baada ya Mseti kukata rufaa kesi iliendelea na mwaka 2015 hakimu wa mahakama hiyo aliyejulikana kwa jina la Mayeye. S. M alitoa ushindi kwa Mseti na wale walioshinda Baraza la Kata wakashindwa,” alisema Mang’era.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji, Chacha Fanusi alikiri kuwepo kwa mgogoro huo, huku akishangaa kuona maeneo ya wajane hao yakichukuliwa wakati hawakuwamo katika kesi.

Ofisa Ardhi wa Halmashuari ya Wilaya hiyo, Privatus Mafuru alikiri kuwepo kwa mgogoro huo na tayari ofisi yake imetoa maelekezo kwa walalamikaji wafike ofisini wakiwa na vielelezo vyote ili wasaidiwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles