24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Waitara ahojiwa na kamati ya maadili kwa saa mbili

Derick Milton, Mara

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita waitara amehojiwa kwa muda wa saa mbili na kamati ya maadili ya chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa mara kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Kati ya tuhuma hizo waitara anadaiwa kuanza harakati za kutangaza nia ya kugombe jimbo la Tarime kabla ya muda, ambapo mbali na yeye viongozi wengine watatu wa chama hicho wamehojiwa na kamati hiyo leo.

Waitara aliwasili kwenye ofisi za chama hicho zilizopo mtaa wa uwanja wa ndege kamunyonge majira ya saa nne asubuhi, na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama hicho mkoa.

Kabla ya Waitara kuhojiwa Kamati hiyo ilianza zoezi la kuwahoji viongozi wengine majira ya saa tano, akiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Serengeti na Katibu wake, kisha akafuatiwa Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime.

Zoezi la kuanza kumhoji Waitara limeanza majira ya 10:50 jioni, na kumalizika saa 1:00 usiku.

Mara baada ya kuhojiwa Waitara hakutaka kuongea na waandishi wa habari huku mwenyekiti wa kikao hicho naye akigoma kuongea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles