DHAKA, BANGLADESH
WAUMINI wa dini ya Kiislamu saba ambao ni wafuasi wa itikadi kali wamehukumiwa kifo na mahakama ya Bangladesh kuhusiana na shambulio la kikatili la mwaka 2016 katika mgahawa mmoja mjini Dhaka, lililoua watu 22.
Mgahawa huo ambao hutembelewa zaidi na watu kutoka mataifa ya magharibi miongoni wa watu hao 22 waliouawa 18 walikuwa ni wageni.
Wengi waliouawa katika shambulio hilo lililodumu kwa saa 12 walikuwa ni raia kutoka nchi za Italia na Japan.
Mahakama imesema lengo lao lilikuwa kuliyumbisha taifa hilo lenye wakaazi milioni 168 Waislamu na kulifanya taifa hilo kuwa taifa la wanamgambo.
Mwendesha mashitaka mkuu wa Dhaka Abdullah Abu amewaambia waandishi habari kuwa washitakiwa saba wamehukumiwa kifo na mmoja ameachiliwa huru.
Shambulio hilo la Julai 2016 lilishuhudia vijana ambao waliokuwa na bunduki na mapanga wakizingira mgahawa huo katika eneo linalokaliwa na watu wa kipato cha juu mjini Dhaka la Gulshan.
Shambulio hilo lilidaiwa kufanywa kundi la Islamic State (IS), lakini Bangladesh haikuwahi kueleza juu ya hilo badala yake waliwashikilia kundi la ndani la kipiganani kwa kuhusika na shambulio hilo.
Watu wote wenye silaha waliuawa na polisi.
Pamoja na hayo kabla ya Mahakama kutoa hukumu dhidi ya watu hao, Waendesha mashtaka walieleza kuwa walithibitisha pasipo shaka yeyote kwamba watu hao walihusika katika tukio hilo.