24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waislamu Iramba wamuahidi kura Magufuli

Na SEIF TAKAZA-IRAMBA

WAUMINI wa Dini ya Kiislamu Mkoani Singida wameahidi kumpigia kura Dk. John Magufuli katika uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika  Oktoba 28 mwaka huu kutokana na kazi nzuri aliyoifanya miaka mitano  ya kwanza.

Ahadi hiyo ilitolewa juzi katika risala ya waumini wa dini ya Kiislamu katika hafla ya Baraza la Eid el  Haj kimkoa lililofanyika  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba  mjini hapa ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula.

Risala hiyo iliyosomwa na Athumani Dule kwa niaba ya Katibu wa Mkoa wa Singida, Alhaj Burhani Mlau na ilisema kuwa; “Waumini wa dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Singida wana imani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jemedari Dk. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kujenga uchumi wa Tanzania hadi kufikia uchumi wa kati kwa kipindi cha muda mfupi tangu aingie madarakani”.

Katika risala hiyo waumini hao wamemwomba Mkuu wa Wilaya hiyo, Emmanuel Luhahula  awapelekee  salamu zao za pongezi  kwa Rais Magufuli  kwa kufanya kazi kubwa ya maendeleo katika nyanja zote ikiwemo kutoa elimu bure, kujenga zahanati, vituo vya afya, kujenga barabara za lami na miundo mbinu mbalimbali, hospitali za wilaya,  mkoa pamoja kuboresha hospitali za rufaa kwa kununua vifaa tiba vya kukidhi mahitaji ya msingi.

Aidha waumini hao walimpa pole kwa msiba mkubwa uliotokea nchini  wa Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Wiliam Mkapa kilichotokea Julai 24 mwaka huu.

 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema risala iliyosomwa mbele yake imempa faraja kubwa kwa heshima ,  kumjali na kumpongeza Rais Magufuli.

“Ndugu zangu waumini ya dini ya Kiislamu na viongozi wa madhehebu mengine  walioshiriki katika hafla hii pamoja na kamati ya usalama ya wilaya hii nashukuru kwa moyo wa dhati kwa kunipa heshma hii ya kuwa mgeni rasmi katika hafla hii inanipa faraja kubwa kwa  kuonesha uhusiano mzuri kati ya uongozi wa Bakwata mkoa na wilaya  na Serikali  kuamua ibada hii kufanyika wilayani kwangu . 

“Lakini pia Kumpongeza Rais wetu Dk. Magufuli na kuahidi kumpa kura katika uchaguzi Mkuu utakaofanyka Oktoba 28 mwaka huu’’ alisema Luhahula

‘’ Ahadi  yenu mlioitoa kwa kumpa kura Rais  Magufuli iwe pamoja na kuwapa kura wabunge na madiwani  katika uchaguzi huo itatupa faraja kubwa kwani mtakuwa mmetimiza ahadi yenu’’ alisisitiza DC Luhahula

Naye Mjumbe Baraza la Masheik Mkoa wa Singida, Alhaj Omar Hassan ambaye pia Imamu Mkuu wa Msikiti wa Taqwa mjini Kiomboi alilishukuru Baraza la Mashekh Mkoa kwa heshima kuupa Msikti wa Taqwa kusali Eid el Haj na kufanya baraza la Eid el Haj kufanyika katika mji wa Kiomboi.

“Kwa heshma na taadhima  sisi waumini wa Msikiti huu tunaishukuru Bakwata Mkoa kwa  kutupa heshima kubwa ya kuaandaa Eid el Haj na Baraza la Iddi  kwa niaba ya Wilaya hii lakini pia tunakushuru wewe binafsi  Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Emmanuel Luhahula kuja kuungana nasi pamoja na viongozi wa dini mbalimbali waliohudhuria hafla hii Mwenyeezi Mungu awabariki sana.

“Pia tunamwombea dua  Rais Magufuli, Mwenyeezi Mungu ampe umri mrefu na afya njema yeye na familia yake pia  tunaahidi tunampa kura zote za ndiyo yeye pamoja na  wabunge na madiwani  waweze kushinda kwa kishindo katika  uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles