24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 25, 2022

Wairani saba kortini kwa kusafirisha dawa za kulevya kilo 859

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Raia saba wa Iran akiwemo Kaptain Jan Miran (42) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine na methamphetamine zenye uzito wa kilo 859.36.

Washtakiwa hao wamepanda kizimbani leo mbele ya Hakimu
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Maria Bantulayne na kusomewa mashtaka na mawakili wa Serikali, waandamizi Joseph Maugo na Juma Maige.

Upande wa Jamhuri uliwataja washtakiwa kuwa ni Miran, Issa Ahmad(30), Amir Kasom (35), Salim Baluch (20), Ikbar Mohammed (22), Mustapha Barksh( 20) na Jamid Mohammed (19).

Inadaiwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mawili ambapo katika shtaka la kwanza wanadaiwa Aprili 23 mwaka huu katika Bahari ya Hindi maeneo ya Mkoa wa Lindi washtakiwa walikamatwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroine yenye uzito wa kilo 504.36.

Katika shtaka la pili wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Methamphetamine yenye uzito wa kilo 355.0.

Baada ya kusomewa mashtaka washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo ya Uhujumu uchumi.

Watuhumiwa wamerudishwa rumande hadi Mei 14, inakapokuja kwa kutajwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,160FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles