27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wairan nchini wakumbuka miaka mitatu ya mauaji ya Soleimani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Diital

WAIRAN nchini wamefanya hafla ya kumbukizi ya mwaka wa watatu ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jenerali Qasem Soleimani, yaliyofanywa na Serikali ya Marekani mwaka 2020.

Hafla hiyo imefanyika jana katika ofisi za Kituo cha Utamaduni cha Irani na kuongozwa na Mkurugenzi wa Kituo hicho, Morteza Pirani.

Mkurugenzi alisema ilikuwa asubuhi ya Januari 3, 2020 wakati habari za kitendo cha jinai cha kuuawa kwa mmoja kati ya makamanda wakuu wa mapambano dhidi ya ugaidi, ilipotangazwa.

“Jenerali Qasem Soleimani aliuwawa karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq pamoja na baadhi ya wasaidizi wake, akiwemo Abu Mahdi al-Mohandes, Naibu Mkuu wa harakati ya wananchi wa Iraq ya al Hashdu al Shaabi.

“Mtazamo wa maadui ulikuwa kwamba, kwa kumuuwa Jenerali Qasem Soleimani itawezekana kusimamisha kasi ya kuendelea kupata nguvu kambi ya muqawama ndani ya nchi na katika ngazi ya eneo la Asia Magharibi.

“Kuuawa Kamanda Soleimani hakukusimamisha au kudhoofisha mapambano dhidi ya ubeberu na Uzayuni, kinyume chake, siku mbili tu baada ya jinai hiyo, Bunge la Iraq liliidhinisha mpango wa kuwafukuza wanajeshi wa Marekani nchini humo na Januari 24 mamilioni ya Wairaqi walifanya maandamano ambayo yalikuwa hayajawahi kushuhudiwa nchini humo dhidi ya Marekani,”alisema.

Alisema mapigano kati ya makundi ya muqawama na Jeshi la Marekani yaliongezeka na kuwa jambo la kila siku nchini Iraq na Serikali ya Marekani ililazimika kuanza duru mpya ya mazungumzo na Serikali ya Baghdad kuhusu hali ya wanajeshi wake miezi mitano tu baada ya kuuawa shahidi Jenerali Soleimani, mazungumzo yaliyobadilisha uwepo wa Jeshi la Merekani nchini Iraqi kutoka hali “vita” na kuwa na sifa ya”ushauri”.

“Hata hivyo kama Marekani ilikubali kushindwa nchini Afghanistan na kuwaondoa wanajeshi wake kwa madhila nchini humo, hivi karibuni pia italazimika kuwaondoa wanajeshi wake wote nchini Iraq,”alisema.

Alisema hali hii inaashiria kwamba baada ya mauaji ya kigaidi ya Kamanda Soleimani, Asia Magharibi in

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles