29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 18, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waimbaji wa Injili waaswa kutojihusisha na muziki wa kidunia

Na Mwandishi Wetu

Mtumishi wa Mungu ndg Alex Msama Amewaonya waimbaji wote wa nyimbo za injili Ambao wamekuwa wakishiriki kwenye majukwaa na wasanii muziki wa kidunia, kwani kufanya ivo ni kushiriki kwenye kumtukuza shetani.

Hayo amebainisha mapema hii leo wakati akizungumza katika mahojiano na chombo kimoja cha habari ambapo amesema idadi kubwa ya wasanii wa injili wamekuwa wakipenda muziki wa kidunia jambo ambalo ni tofauti na makusudio ya Mungu ya kuwabariki vipaji vya vya kumtumikia.

Pia amewataka wasanii hao kuacha tamaa ya pesa ambayo inawapelekea wasanii hao kwenda kushiriki kwenye majukwaa ya muziki wa kidunia,

“Nawaonya waache kushiriki madhabahu za shetani,2 Wakorinto 6: 14-18 Msiambatane pamoja na watu wasioamini, pia wajihadhari na kupenda pesa kwani pesa nyingine ni za maagano ya kuzimu” Alex MSAma

Alex Msama ni mdau mkubwa wa Muziki wa Injili na Hivi karibuni alipokea tuzo ya heshima ya kuwa muandaaji bora wa matamasha ya injili nchini Tanzania ambayo maarufu yalikuwa yanafahamika kwa jina la TAMASHA LA PASAKA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
594,000SubscribersSubscribe

Latest Articles