25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 4, 2022

Contact us: [email protected]

Waigizaji walioamua kuishi na samba ndani

simbaJOSEPH HIZA, DAR ES SALAAM

NI nadra kwa mwanadamu kuishi na wanyama hatari wa mwituni katika makazi yao kana kwamba ni wanyama wafugwao kama mbwa na paka.

Lakini mfululizo wa picha hizi za miaka ya 1970 unaonesha familia ya waigizaji wakiishi na simba waliyempa jina la Neil.

Hata hivyo, hilo haliondoi ukweli kwamba funzo walilipata.

Ni simulizi inayotufundisha kuwa bila kujali kiasi gani tunawapenda au kupatwa na hisia za ajabu kwa ukaribu nao, kamwe hatutaweza kufahamu vyema kinachoendelea ndani ya ubongo wa mnyama hawa wa wa mwituni.

Baada ya ziara yake barani Afrika, mwigizaji Tippi Hedren, mumewe Noel Marshall, na binti yao pia mwigizaji Melanie Griffith, walitaka kutengeneza sinema kuhusu simba baada ya kuwaona kwa macho yao.

Mkufunzi wa wanyama ambaye alikuwa akimiliki simba Ron Oxley, aliwapa ushauri kwamba ili kufanikiwa azma yao wanapaswa kuwafahamu vyema kwa kuishi na simba.

Hivyo waliishia kumchukua simba waliyempa jina la Neil ili kuishi naye nyumbani.

Maisha yao yakatengenezwa kipindi na mpiga picha Michael Rougier.

Maisha yao na Neil yalionekana mazuri, lakini filamu yao, Roar yaani Nguruma, haikwenda vizuri sana.

Melanie alihitaji kushonwa nyuzi 50 baada ya kushambuliwa na simba jike wakati wa upigaji filamu.

Na mpiga picha Jan de Bont aliazimika paji lake la uso kuchonwa baada ya kufumuliwa na simba hao.

Watu 70 walijeruhiwa wakati wa utengenezaji filamu hiyo iliyohusisha paka hao wakubwa hatari 150. Filamu hiyo iligharimu zaidi ya dola milioni 17.5 lakini ilitengeneza dola milioni mbili.

Wakati familia hiyo ikiwa kamwe haikuraruliwa na Neil, usiku mmoja mnyama huyo alimshambulia mmiliki wake Ron Oxley wakati wa sherehe ya chakula cha usiku kwa wageni wake kutoka Uingereza katika nyumba yao.

Wawili hao waligaragazana jikoni huku simba akiparura makucha yake makuwa na Oxley kujaribu kumdhibiti na kujinasua.

Mwishowe Neil alijiondoa kutoka mwili wa Okley lakini akitoa sauti kali ya kuunguruma na kutoka katika nyumba hiyo.

Melanie kwa sasa ana umri wa miaka 59 alikuwa na umri wa miaka 14 wakati alipoondokea kuwa kipenzi zaidi cha Neil, akilala na kucheza naye huko Sherman Parks , California.

Picha za Melanie na mama yake wakiwa wanacheza na simba huyo ziliwekwa kwenye jarida la ‘Life Magazine‘ mwaka 1971 ambapo zilikua zinaonesha mtoto huyo kuwa na ukaribu mkubwa na Simba na hata kulala na kuogelea nae.

Mama Melanie aliyeigiza kwenye filamu ya ‘The Birds’ miaka minane baada ya kupigwa kwa picha hizo alionekana pia kupenda kucheza na mnyama huyo pori waliyemchukua kutoka nyumba inayotunza simba, ambao walionekana hawana makazi mazuri.

Alipenda kulala zaidi katika kitanda cha Melanie na katika usiku mmoja wazazi wa Melania waliwakuta wawili hao wamelala pamoja huku mdomo wa Neil ukiwa futi zisizozidi mbili kutoka mwili wa binti huyo.

Griffith alielezea jinsi alivyopata alama za usoni na kusema Simba huyo hakumaanisha kumuumiza, aliendelea kusema ‘Baada ya kukaa miaka saba na Simba unasahau kama Simba ni mnyama na pia ni hatari kuwa nao karibu, katika utengenezaji wa filamu hamna mnyama aliyeumia ila waigizaji wengui waliumia na kukimbizwa hospitali’

Mama wa Griffith ambaye sasa ana miaka 87 awali alipendezwa sana na uhusiano wa Griffith na wanyama mpaka akaamua afungue kituo cha kulea wanyama ambao wamekosa malezi kiitwacho ‘Shambala Preserve’ kwenye mjia wa Acton California Marekani mwaka 1972.

Hata hivyo kwa sasa anakiri kitendo cha kumwacha bintiye mdogo kipindi kile alale na kucheza na simba pamoja na kumleta katika makazi yao ni moja ya kipuuzi kuwahi kuyafanya.

“Licha ya kwamba hatukuraruliwa na simba, huwezi jua siku moja unaweza kugeuka asusa kwa wanyama hawa hatar. Hakika nikiziangalia picha zile mwili unanisisimka kwa hofu,” alisema.

“Ulikuwa ujinga kwa kweli kumfanya mnyama pori mwenye uzito wa lb 400 kuwa kama mnyama wa nyumbani kwani angeweza kuniua au kuiua familia yangu wakati wowote,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,544FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles