29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wahisani wakubali kuchangia bajeti

Saada Mkuywa Naibu Waziri wa FedhaSHAMIMU MATTAKA (DACICO)
HATUA zilizochukuliwa na serikali dhidi ya waliochota zaidi ya Sh bilioni 200 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zimesaidia Tanzania kukubaliwa kupewa Sh bilioni 71 na wahisani wa Maendeleo katika bajeti ijayo ya 2015/2016.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alisema Dar es Salaam jana kwamba wahisani hao wamefikia hatua hiyo baada ya kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali dhidi ya watuhumiwa.
“Baada ya suala hilo Tanzania ilikuwa katika sura ambayo si nzuri lakini baada ya kuwachukulia hatua wamekubali kusaidia bajeti ya 2015/2016 na wale wanaohusika na tuhuma nyingine kubwa,” alisema.
Mkuya alisema wahisani waligoma kuchangia bajeti ya serikali katika mambo mbalimbali huku wakichangia asilimia tano pekee katika bajeti ya ujumla.
“Tayari wahisani wameshatoa Dola za Marekani milioni 114 na sasa wamejipanga kuchangia bajeti ya mwaka ujao katika nyanja mbalimbali Dola milioni 44 (sawa na Sh bilioni 71) ambazo zilikuwa ni sehemu ya Dola milioni 500,” alisema Mkuya.
Waziri alizitaja Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kuwa tayari zimetangaza kutoa msaada wa Dola milioni 227 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa bajeti ya 2015/16.
“Benki ya Dunia imekubali kuchangia asilimia 17 ya bajeti ya serikali ambayo ndani yake kuna vipengele tofauti vinavyohusu msaada wa bajeti ya jumla, miradi na nyingine.
“Misaada hii yote iliathiriwa na hili suala la Escrow ikiwamo asilimia tano ya bajeti ambayo ilicheleweshwa kutolewa kwa sababu hiyo, lakini leo tumekwamuka na kuahidiwa kupewa,” alisema Mkuya.
Asilimia 80 ( Sh bilioni 922) ni ahadi ambazo zilikuwa hazijatolewa na wahisani wa maendeleo katika vipengele vyote vya bajeti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles