29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wahariri kujadili Muswada Sheri ya Habari katika kongamano 12

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wanatarajia kutumia Kongamano la 12 la Kitaaluma linaloandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) mjini Morogoro kujadili Muswada wa Sheri ya Huduma za Habari.

Ikumbukwe kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ulisomwa bungeni kwa mara ya kwanza Machi 10, mwaka huu.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF, Neville Meena(katikati) akizungumza wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari.

Akizunguza mapema leo Machi 27, 2023 mjini Morogoro Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF, Neville Meena amewaambia Waandishi wa Habari amesema kongamano hilo ambalo litafunguliwa na Machi 29, na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, litatoa mwanya pia kwa wahariri kujadili muswada wa sheria ya huduma za habari.

“Katika kongamano hili la 12 ambalo litafunguliwa Machi 29, na Mheshimiwa Waziri Nape Nnauye, Wahariri watatumia fursa hiyo kujadili muswada wa sheria ya huduma za habari ambao tayari umeshasomwa bungeni.

“Na ndiyo sababu utaona kuwa pamoja na mambo mengine tumemualika Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Nbumbaro, hivyo watajadili na kuona ni kwa namna gani tutapata mawazo chanya juu mabadiliko haya tunayoyaendea,” amesema Meena.

Mbali na hilo Meena amezitaja mada nyingine kuwa kutakuwa na mada sita ambazo ni Utendaji wa Vyombo vya Habari, Taaluma na Maadili; Wanawake katika habari na hatari ya kutoweka kwao kwenye vyumba vya habari.

Mada nyingine kuwa ni Uchumi wa Vyombo vya Habari na jinsi ya kuvinusuru; Mabadiliko ya Teknolojia, Ukuaji na Ujenzi wa Mitandao ya Kijamii yenye viwango vya kitaaluma; Mchakato wa Mabadiliko ya Sheria za Habari na mweleko wake.

Deus Kibamba.

Akizungumza hivi karibuni katika kipindi cha Kipima Joto cha ITV juu ya hatua ya mabadiliko iliyofikiwa hadi sasa, Deus Kibamba ambaye ni Mjumbe wa Umoja wa Wadau wa Haki ya kupata Taarifa(CORI) amesema kuwa: “Nadhani tunaona mwanga na moshi mweusi mchanganyiko, sababu mswada wenyewe unaoletwa mambo yaliyomo yanaleta mwanga na hivyo yanazidi kuongeza uchanya kwenye sheria, hivyo hilo hatuwezi kukidharau hata siku moja.

“Sisi kama wadau wa sekta ya habari tunadhani kwamba hata ingekuwa ingekuja kufungu kimoja kimenyooshwa kutoka palipopinda bado tungeshukuru.

“Lakini tunachojaribu kusema ni kwamba hivi vifungu ambavyo Serikali inaleta kwa ajili ya kuvirekebisha ni vichavhe mno ikilinganishwa na sheria yenyewe ilivyo na mapungufu, hivyo tunashukuru na tunaendela kushukuru kwa hatua hii ilivyofikiwa, kwani yoote yaliyoletwa kwenye muswada huu yanaongeza uchanya,” amesema Kibamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles