23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Wahamiaji kutoka Libya waingia Rwanda

KIGALI, RWANDA

KUNDI la wahamiaji 66 linalojumuisha watu walio hatarini zaidi pamoja na watoto walio peke yao limewasili nchini Rwanda kutoka Libya, Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi (UNHCR), limesema.

Miongoni mwa watu hao ambao baadhi yao wanatoka mataifa ya Afrika, ni mtoto wa miezi miwili mwenye asili ya kisomali aliyezaliwa katika kituo cha kuwazuilia wakimbizi nchini Libya.

Msemaji wa UNHCR kanda ya Afrika, Charlie Yaxley ameiambia BBC nchini Rwanda kuwa shirika hilo litawatafutia stakabadhi za kuomba hifadhi wale ambao wanataka kuishi Rwanda au kuwasaidia wale wanaotaka kurejea makwao.

“Nchini Rwanda tutawapatia chakula, maji, malazi na mahitaji mengine ya muhimu. Tuna watalaam tisa watakaowasaidia kupona kiwewe cha yale waliyoyapitia Libya” Yaxley amesema.

Wahamiaji hao wataishi katika kituo cha muda kilichopo umbali wa saa moja kwa gari kutoka mjini Kigali.

Akitoka katika kituo cha ukusanyaji wa wahamiaji cha Libya , Daniel mmoja wa wahamiaji katika kundi lilililohamishiwa Rwanda aliiambia BBC wiki iliyopita kuwa wanafurahia kuondoka Libya.

“Tulipokuwa tunaweka sahihi ya kidole tuliona barua inayosema tunaondoka kuelekea Rwanda na tukajihisi ni kama tulikuwa tunatengana na kifo “

Zaidi ya wahamiaji 4,500 wanashikiliwa katika mahabusu baada ya ndoto yao ya kuvuka bahari ya Mediterranean kuelekea ulaya kukatizwa.

Rwanda ilikubali kuwahfadhi wahamiaji 500 kwa ushirikiano na UNHCR, na Muungano wa Afrika ulitoa hakikisho la usafiri wao wa kutoka Libya kuelekea Rwanda , ili kuwaepusha na hatari ya kushambuliwa kwa roketi na kubakwa . Haijafahamika wazi ni kwa muda gani wahamiaji hao watakuwa Rwanda na wana uhuru kwa kiwango gani kuondoka nchini humo

Maafisa wanasema miongoni mwa wahamiaji hao 66 ni wanawake na watoto walio katika hali mbaya kiafya na vyombo vya habari vilidhibitiwa kuwaona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles