24.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Wahadhiri wa Kigeni wapungua

Ramadhan Hassan, Dodoma

Serikali imewapunguza wataalamu 502 walioajiriwa kutoka vyuo vikuu 17 hadi kufika 151 katika miaka 10 iliyopita kati ya 2008-2009 hadi 2018-2019.

Hayo yameelezwa Leo Mei 24 bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)Mwita Waitara kwa niaba ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.

Waitara alikiwa akijibu swali la Mbunge wa Nkenge,Dk.Diodorus Kamala(CCM).

Katika swali lake,Kamala alitaka kujua katika miaka 10 iliyopita wahadhiri wangapi wameajiriwa katika Vyuo Vikuu nchini.

Akijibu,Waitara amesema Vyuo Vikuu vimekuwa vikiajiri wataalamu kutoka nje kwa malengo ya kuboresha hali ya taaluma na kujiimarisha katika masuala ya kiutafiti katika nyanja mbalimbali.

“Ajira ya wataalamu wa kigeni hutolewa kwa kibali maalum na kwa mkataba na kwa kuzingatia mahitaji maalum yaliyopo katika Vyuo husika,” amesema.

Waitara amesema katika miaka 10 iliyopita kati ya 2008-2009 hadi 2018-2019 Vyuo Vikuu 17 viliajiri wataalamu wa kigeni 502 ambapo Serikali imewapunguza hadi kufikia 151.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles