25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wagonjwa wahamishwa Hospitali ya Amana kupisha wenye corona

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

WAGONJWA wote waliokuwa wakipata huduma katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam, wamehamishwa  ili itumike kutoa huduma za afya kwa wagonjwa wa corona (COVID – 19).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Zainab Chaula, akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo jana alipotembelea majengo yatakayotumika kuwalaza wagonjwa wa corona, alisema wagonjwa waliokuwa wanapata huduma katika hospitali hiyo wamehamishiwa katika hospitali nyingine za Serikali jijini Dar es Salaam. 

Alisema Serikali imetoa kiasi cha Sh milioni 200 kwa ajili ya ukarabati mdogo wa baadhi ya majengo ya hospitali hiyo.

Dk. Chaula aliwataka watumishi wa sekta ya afya kukumbuka kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuvaa vifaa vya kujikinga na maambukizi wakati wa kuwahudumia wagonjwa wa COVID-19 hospitalini hapo. 

Aliwakumbusha watumishi wa sekta ya hiyo kutimiza wajibu wao katika kipindi cha janga la corona huku wakizingatia kiapo cha utii wa majukumu yao ya utoaji huduma za afya kwa wagonjwa.

Alisema Serikali ipo tayari kuwezesha huduma za afya kutolewa kikamilifu kwa wagonjwa wa corona nchini na kuwa wizara hiyo itafanya juhudi kupunguza maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo nchini.

Ijumaa wiki hii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema Serikali imeelekeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kuacha kupokea wagonjwa wenye dalili wa corona ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma za kibingwa na bobezi kwa wagonjwa wa magonjwa mengine nchini.

Alisema badala yake Serikali Hospitali ya Amana itatumika kama kituo maalum cha matibabu ya ugonjwa wa CODIV-19. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles