30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wagonjwa wa macho washauriwa kupata tiba

WNa Nathaniel Limu-SINGIDA

ASILIMIA 94 ya watu wenye matatizo ya macho mkoani Singida wanaofika kwenye vituo vya afya wakipata matibabu sahihi na kwa wakati, wana uwezekano mkubwa wa kupona.

Lakini asilimia sita ya wagonjwa wa macho wanaofika kwenye vituo vya afya, uwezekano wa kupona ni mgumu.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Mtaalamu wa Macho ambaye pia Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida, Dk. Ng’hungu Kuzenza, katika hafla fupi ya kupokea msaada uliotolewa na Waislamu wa dhehebu la Shia ambao wametoa msaada wa kugharamia matibabu na upasuaji kwa wakazi 100 wasiokuwa na uwezo wa kulipia tiba ya macho.

Dk. Kuzenza alisema chanzo kikuu kinachosababisha matatizo ya macho ni uchafu, hivyo aliwataka wananchi kuwa makini kulinda macho kwani ni kiungo muhimu katika maisha ya binadamu.

Mtaalamu huyo aliwapongeza Waislamu hao wa Shia kwa kuiunga mkono Serikali katika kutoa huduma ya afya, ikiwemo kwa watu wenye matizo ya macho.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Madrastu Al-Wahadar, Sheikh Abdulkarimu Nkusui, alisema dhehebu  la Shia Thnashariya chini ya Taasisi yake ya  Sayyidi Shuhadaa mkoani Singida, limegharamia huduma ya upimaji na matibabu ya macho kwa wakazi zaidi ya 100 wasio na uwezo.

Alisema lengo ni kuwasaidia wagonjwa wa macho wasio na uwezo wapone, warejee kushiriki katika shughuli za maendeleo yao binafsi na ya taifa kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles