28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Wagonjwa wa corona nchini wafikia 19

AVELINE KITOMARY, DAR ES SALAAM

Idadi ya Wagonjwa wanaougua homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona  (Covid-19) imeendelea kuongezeka kutoka 13 na kufikia 19.

Taarifa iliyotolewa na waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu zimesema kuwa wagonjwa hao wamegundulika baada ya kufanyiwa vipimo katika maabara ya Taifa.

“Ninapenda kutoa taarifa kuwa leo Machi 30, tunathibitisha kuwepo kwa wagonjwa wapya watano wa Covid-19 baada ya kufanyiwa vipimo katika maabara ya Taifa, Kati ya wagonjwa hawa watatu ni kutoka Dar es salaam na wawili kutoka Zanzibar.

“Hivyo sasa jumla ya wagonjwa wa Covid -19 nchini ni 19 akiwemo mgonjwa mmoja ambaye aliyetolewa taarifa na waziri wa Afya wa Zanzibar Machi 28 mwaka huu.

Katika taarifa hiyo waziri Ummy alianisha wagonjwa waliko Dar es salaam ambapo wanaume ni wawili na mwanamke mmoja.

“Mwaume (49) Mtanzania alikutana  na raia kigeni kutoka miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi, mwingine ni mwanamke (21), Mtanzania ambaye ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa na mwaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia ni miongoni mwa watu wanaofatiliwa,”amesema.

Hata hivyo waziri Ummy amesema kuwa kazi ya kuwafatilia watu wa karibu wote waliokutana na wagonjwa hao bado inaendelea na kuwataka wananchi waendelee kuchukua tahadhari ili kujikinga na virusi hivyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles