21.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Wagonjwa 43,000 wafanyiwa upasuaji MOI ndani ya miaka minne

Na AVELINE KITOMARY

JUMLA YA wagonjwa 43,200 wamefanyiwa upasuaji wa kibingwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) katika kipindi cha miaka minne cha Uongozi wa Rais Dk John Magufuli kutokana na maonesho ya huduma mbalimbali hasa za kibingwa.

Akizungumza Na waandishi wa leo Novemba 22 Mkurugenzi wa MOI Dk Respicious Boniface amesema amesema huduma hizo zimeweza kuokoa maisha ya Watanzania wengi ambapo idadi ya wagonjwa wa upasuaji kutoka 400 hadi 500 kwa mwezi hadi 700 mpaka 900 kwa mwezi.

“Wagonjwa 900 walibadlisha nyonga,kubadilisha magoti 870,upasuaji wa mfupa wa kiuno watu 618 wamepata huduma kuna upasuaji wa ubongo tayari watu 880 wameshapata huduma na watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi walikuwa 2,070.

“Katika huduma zingine kama dawa zote muhimu kwa matibabu zinapatikana kwa asilimia 95 na tunategemea kufungua Community pharmacy hivi karibuni ili kuhakikisha dawa zote zinapatikana kwa asilimia 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,580FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles