Kigali, Rwanda
RAIS Paul Kagame wa Rwanda anatarajiwa kuchuana na wanasiasa wawili katika uchaguzi mkuu nchini humo utakaofanyika mwezi ujao.
Tume ya uchaguzi nchini Rwanda imewaidhinisha wagombea wawili wa upinzani kupambana na Kagame wakati wa uchaguzi mkuu huo, baada ya wagombea wengine akiwamo mwanamke pekee kushindwa kutimiza masharti.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Tume ya Uchaguzi  ya Rwanda, Profesa Kalisa Mbanda alisema kwamba wanasiasa kutoka upinzani waliokidhi vigezo vya kuwania urais ni pamoja na Frank Habineza wa chama cha Democratic Green Party na mgombea binafsi Philippe Mpayimana
Taarifa zaidi zinasema kuwa, Gilbert Mwenedata, Fred Barafinda Skikubo na mwanamke wa pekee Diane Rwigara hawakufanikwia kuidhinishwa baada ya kushindwa kupata saini 600 za wapiga kura kama inavyotakiwa kikatiba.
mwisho
CAPTION: Polisi wa nchini Burundi wakipiga kijana mdogo