24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WAGENI ILALA KUORODHESHWA KWENYE DAFTARI MAALUMU

 

FRANK KAGUMISA (SAUT) Na NORA DAMIAN – DAR ES SALAAM


MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa kuwaorodhesha wananchi wanaofika kwenye mitaa yao katika daftari maalumu  kubaini wahalifu na wahamiaji haramu.

Mjema  alifanya ziara katika kata 13 za jimbo la Ukonga kuanzia Agosti 13 hadi 18 kusikiliza kero za wananchi na kubaini kuwa baadhi ya maeneo watu wanaonekana usiku tu.

Akizungumza jana wakati wa kutoa tathmini ya ziara hiyo, alisema imebainika maeneo mengine watu wanaishi lakini hawajulikani wanafanya shughuli gani.

“Kila mwenyekti wa serikali ya mtaa ahakikishe anawajua wakazi wake na kama mgeni amekuja lazima aulizwe atakaa eneo husika kwa muda gani na amekuja kufanya nini.

“Hii itasaidia sana kupunguza uhalifu na wahamiaji haramu ambao wengi huja na silaha,” alisema Mjema.

Alisema mkakati huo unalenga kupunguza uhalifu katika ngazi ya mitaa kwa vile  kumekuwa na matatizo ya wananchi kutishiwa, kukabwa na kuibiwa mali zao.

“Kuna watu wengine wanaonekana usiku tu,  je, mchana wanakuwa wapi kwa hiyo ni kazi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa kuwajua,” alisema.

Kuhusu kero, alisema katika ziara hiyo aliweza kutatua papo kwa papo kero 606 zinazohusu miundombinu ya barabara, afya, ulinzi na usalama na kero za kawaida.

Kwa mujibu wa DC huyo, kero 20 zikiwamo za sekta ya ardhi walizibeba kwa sababu  zilikuwa zikihitaji majibu ya wizara ambako mawaziri husika imeahidi kabla ya mwisho wa mwezi huu itazitatua.

“Kero nyingi za wananchi ambao wako kwenye mitaa hazijasikilizwa kwa kiasi ambacho tunategemea kifanyike.

“Maswali na kero nyingine wala zilikuwa hazihitaji mkuu wa wilaya aende bali yangeweza kumalizwa na viongozi walioko kwenye maeneo husika,” alisema.

Aliwataka watendaji wa kata na mitaa wahakikishe wanatatua kero kwa kuteremka chini kufanya vikao na wananchi na zile zitakazokuwa nje ya uwezo wao wazi[eleke  ngazi ya tarafa au wilaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles