26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wagangambaroni kwa tuhuma za mauaji ya albino

Kadama Malunde, Shinyanga na Renatha Kipaka, Bukoba
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga limewatia mbaroni waganga wa tiba asilia 26 katika Wilaya za Kishapu, Shinyanga na Kahama o kupiga ramli za uchonganishi na kusababisha mauaji ya albino.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, alisema operesheni ya kuwakamata waganga hao ilianza Machi mosi hadi Machi 9 mwaka huu, na baadhi ya waganga hao wamo wanaojihusisha na mauaji ya vikongwe.
Alisema kabla ya kuwakamata waganga hao yalifanyika mahojiano na upekuzi ambako walibainika kujihisisha na upigaji ramli chonganishi na mauaji ya vikongwe na albino.
Katika msako huo waganga hao walikamatwa pia wakiwa na nyara mbalimbali za Serikali, zikiwamo ngozi za fisi, kicheche, nyati, simba, nyegere, korongo na kitovu cha mbweha.
Wanyama wengine waliokamatwa kwa waganga hao ni digidigi, mikia ya nyumbu, pembe na viungo mbalimbali vya wanyama aina tofauti vikiwamo vibuyu vilivyovishwa shanga.
Kamanda Kamugisha aliwataja waganga waliokamatwa kuwa ni Ester Madirisha (65) mkazi wa Mwalukwa, Selekwa Nicholaus (42) mkazi wa Mwang’osha, Siyantemi Jinasa (41) wa Kijiji cha Ibubu, Fatuma Shija (47) kutoka Ngogwa Kahama, Makandi Guma (51) wa Ibubu na Gamaweshi Mayala (49) wa Kijiji cha Lubaga.
Wengine ni Saimon Lukelesha (34), Jidanda Samanya (20) na John Lubanga (28) wote kutoka mkoani Tabora, Samwel Zengo (37) mkazi wa Lagana, Jimoka Jitobelo (93) wa Ibingo, Shija Venji mkazi wa Ibingo Samuye, Milembe Ndahya (50) mkazi wa Isela, Kashinje Nyakali (55) mkazi wa Samuye na Nzela Maige (55) kutoka Isela Samuye.
Alisema katika msako huo watu wanne walikamatwa wakituhumiwa kujihusisha na ukataji mapanga, ambao ni John Sabuni (45) mkazi wa Shinyanga, James Machimanya (34) mfanyabiashara wa Kishapu, Jackson Charles (55) mkazi wa Shinyanga, Juma Ndodi (50) wa Kijiji cha Buyange.
Wengine waliotajwa ni Kashinje Kayila (46), Tabu Salamba (43) wote wakazi wa Kijiji cha Ngaganulwa kata ya Usanda, Itwelyamhela Shija (28), Jilala Maige (44) wote kutoka Kijiji cha Singita kata ya Usanda, Nyanzobe Shija (36), Mbula Maduka (57), Masalu Nkuba (53) na Lugonda Kwangu (45) wote wa Ibadakuli Shinyanga.
Hata hivyo Kamanda Kamugisha alisema hadi sasa polisi wanaendelea kumsaka mganga mmoja, Milembe Shinji, mkazi wa Kijiji cha Ibingo .
Alisema waganga hao watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani Kagera linawashilikia watu 12 kutokana na mauaji ya watu wawili waliouawa Machi 9 mwaka huu, kwa kukatwa mapanga katika eneo la Kitendaguro Manispaa ya Bukoba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henery Mwaibambe, aliwataja waliouawa kuwa ni Emani Gilidi (35) na Evarist Maliseli (30).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles