Wafugaji vipepeo walia na serikali usafirishaji viumbe hai

0
800

Amina Omari, Muheza

Wafugaji wa vipepeo wilayani Muheza mkoani Tanga wameiomba serikali kuangalia upya zuio la usafirishaji wa viumbehai kwani limesababisha athari ya kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa mbele ya Mkuu wa mkoa wa huo Martin Shigela, wakati wa ziara yake katika kata ya Kisiwani wilayani humo.

Mmoja wa wafugaji  Dickson Hoza, amesema kuwa kuzuwa kwa usafirishaji wa vipepeo kumesababisha uchumi wa wananchi kuyumba kwakuwa biashara hiyo ilikuwa ndio tegemeo lao.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kero yetu kubwa ni zuio la usafirishaji wa vipepeo umesababisha shughuli nyingi za kimaendeleo kusimama kutokana na ukosefu wafedha za kuchangia miradi hiyo kwani biashara hiyo ilikuwa ndio kitega uchumi chetu” Hoza.

Hata hivyo Shigela aliwataka kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

“Serikali ilikuwa na nia njema ya kulinda raslimali zetu hivyo niwaombe endeleeni kuvumilia wakati suluhisho la kudumu linakuja”alisema RC Shigela.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here