WAFUASI WA RAIS MADURO WASHAMBULIA WABUNGE VENEZUELA

0
536
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro

CARACAS, VENEZUELA

MAGENGE yanayounga mkono Serikali ya Rais Nicolas Maduro, yamevamia Bunge na kuwashambulia wabunge wa upinzani na kuwajeruhi saba.

Wafuasi hao wa Maduro wasiopungua 100 walivamia Bunge jana na kuwazuia kuondoka kwa saa tisa wabunge 350, wahudumu wa Bunge, wanahabari na wageni.

Polisi waliokuwapo walionekana kutoingilia kati kutuliza vurugu hizo, ambazo zimejiri wakati wabunge hao wakihudhuria kikao maalumu cha kuadhimisha Siku ya Uhuru.

Baadaye wanajeshi na polisi walizingira kundi hilo kuwazuia na kuruhusu wabunge hao kuondoka.

Tukio hilo ni la karibuni katika mzozo wa kisiasa, ambao umeikumba Venezuela kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Watu 90 waliuawa katika maandamano ya karibu kila siku ya kuupinga utawala wa Maduro.

Washambuliaji hao walikuwa wamejihami kwa fimbo, marungu, vipande vya mabomba na wengine bunduki.

Maduro ambaye anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa upinzani, amelaani shambulizi hilo, akisema anajitenga nalo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here