Wafuasi wa Chadema, Cuf watimuliwa mahakamani wakisubiri kesi ya Mbowe, Lipumba

0
1864

Elizabeth Joachim, Dar es Salaam

Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (Cuf) wametimuliwa na polisi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kuanzisha kwa vurugu.

Tukio hilo limetokea mapema leo asubuhi Ijumaa Novemba 30, baada ya Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi ndani na nje ya mahakama hiyo ili kuwadhibiti wafuasi hao kutokana na kesi kubwa mbili zinazotarajiwa kutolewa uamuzi leo.

Kesi hizo ni pamoja na ile iliyofunguliwa na viongozi wa Cuf, wakitaka kujua Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, ni mwenyekiti halali wa chama hicho au la.

Kesi ya pili ile ya maombi ya dhamana ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko ambayo inatarajiwa kutolewa uamuzi kuhusu pingamizi lililowasilishwa na upande wa  Jamhuri la kutaka rufaa itupwe ya kupinga kufutiwa dhamana kwa washtakiwa hao litupwe kutokana kutofuata vifungu vya kisheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here