KATIKA hali iliyozua taharuki, watu watano wameugua na kufariki wakiwa wanasafirisha jeneza la mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa kipindupindu.
Tukio hilo limetokea nchini Nigeria, ambapo mwili wa marehemu ulisafirishwa kwa basi kutoka Kijiji cha Ojota kwenda Sanyinna.
Watano walifika wakiwa wamezidiwa na sasa wanaendelea na matibabu katika Kituo cha Afya cha Sanyinna.
Juu ya tukio lilivyoanza, watu 10 waliokuwa kwenye gari la maiti walianza kuumwa na watano walipoteza maisha kabla ya kufika walikokuwa wanakwenda.