24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wafariki dunia baada ya kunywa dawa ya mganga

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda

Na Walter Mguluchuma, Mpanda

WAKAZI  watatu wa kitongoji cha Senta ya Maradona katika Kijiji cha Kabange mkoani hapa, wamefariki dunia baada ya kunywa dawa waliyopewa na mganga wa kienyeji  kutibu ugonjwa wa tumbo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alikiri kutokea   tukio hilo na kuwataja marehemu hao  kuwa ni Kabula Joseph (23) na Idulu Masanja (30) ambao ni wakwe wa mganga huyo.

Alisema tukio hilo  lilitokea Oktoba 13, mwaka huu nyumbani kwa mganga huyo, Msajigwa  Jaheda (55).

Inaelezwa kuwa Mganga huyo alimpatia mke wa mtoto wake mdogo aitwaye Kabula dawa ya kienyeji ya kusafisha tumbo .

“Baada ya kutenda hayo mganga huyo alitoroka na kujificha kusikojulikana. Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kumtafuta mganga huyo,” alisema Kamanda Nyanda Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda, Dk. Mohamed Mpunja alisema baada  ya kunywa dawa  hiyo, Kabula alitapika na kupoteza nguvu mwilini na  hatimaye alifariki dunia.

“Mtu mwingine aliyepoteza maisha ni Masanja ambaye alifika katika kitongoji hicho kuhani msiba.

“Kabla  ya  kurudi nyumbani kwake alienda kwa mganga huyo wa kienyeji  aitibiwe  tumbo la ngiri.

“Mganga huyo alimpatia dawa ambayo baada ya kuinywa alitapika na kuharisha na kisha alifariki dunia muda mfupi baadaye,” alisema.

Kutokana na tukio hilo, Dk. Mpunja amewataka wananchi mkoani humo  kwenda kwenye vituo vya afya  wanapohisi dalili za ugonjwa wowote ili kupata matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles