30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 31, 2023

Contact us: [email protected]

WAFARANSA WATAKA FILLON AJIONDOE MCHUANO WA URAIS

PARIS, UFARANSA


KARIBU theluthi mbili ya wapiga kura nchini Ufaransa wanataka mgombea urais wa chama cha kihafidhina cha Republican, Francois Fillon ajiondoe kwenye kinyan'ganyiro hicho kutokana na madai kuwa mkewe alilipwa mshahara kwa kazi ambayo hakuifanya.

Utafiti huo uliofanywa na Jarida la Journal du Dimanche la hapa, ambapo jumla ya wapiga kura 1,004 walihojiwa, umeonesha asilimia 65 wangependelea Fillon ajiondoe kwenye kinyan'ganyiro hicho.

Hata hivyo, asilimia 70 ya wafuasi wa Fillon kutoka chama chake cha Republican waliohojiwa katika utafiti huo wanataka aendelee kuwania nafasi hiyo.

Kwa upande wake, Fillon amesema ataendelea kubakia kwenye kinyanganyiro hicho bila kujali kinachoendelea dhidi yake.

Awali wiki kadhaa zilizopita alisema atajiweka kando iwapo atafanyiwa uchunguzi kutokana na kashfa hiyo inayomhusu mkewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles