30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

WAFARANSA WAMTAKA OBAMA KUWANIA URAIS UFARANSA

PARIS, UFARANSA


OMBI la mtandaoni linalomtaka Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama kuwania urais katika uchaguzi mkuu nchini Ufaransa limewavutia takriban wafuasi 42,000.

Mabango ya kampeni yanayosomeka ''Oui, on Peut'' ikimaanisha kaulimbiu ya kampeni ya Obama ‘Ndiyo, Tunaweza’ yametumika mjini Paris.

Hata hivyo, Obama si raia wa Ufaransa na hivyo hawezi kugombea urais.

Lakini wale wanaofanya mzaha huo wanasema lengo lao ni kuonyesha hakuna wagombea wazuri waliojitokeza kuwania urais nchini hapa.

Ujumbe wao kwa wagombea hao kama alivyosema mmoja wa waandaaji wa ombi hilo ni ‘jamani hamfai’.

Wapigakura wa Ufaransa watashiriki katika Uchaguzi Mkuu Aprili 25 na iwapo wagombea hawatapata asilimia 50 ya kura katika raundi ya kwanza, wapigakura watarudi Mei 7 kuamua kati ya wagombea wawili waliopata kura nyingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles