25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

WAFANYIWA UPASUAJI WA KUPANDIKIZA BETRI

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

WATU 15 wamefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu iliyokuwa imeziba huku wengine watatu wakifanyiwa upasuaji wa kupandikiza betri.

Madaktari bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wamefanya upasuaji huo kwa kushirikiana na madaktari kutoka Hospitali ya BLK ya  India.

Akizungumza na waandishi wa habari  hospitalini hapo jana,  Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo wa Hospitali hiyo, Dk. Peter Kisenge alisema watu hao wote wanaendelea vizuri.

“Mmoja kati yao tumemfanyia upasuaji wa kuzibua mishipa yake iliyoziba bila kupasua kifua na hawa tuliowawekea betri ni watu wazima na zitawawezesha kuishi hadi miaka 20,” alisema.

Alisema muda huo utakapomalizika watalazimika kurudi tena hospitalini  wafanyiwe tena upasuaji   kubadilisha betri.  

“JKCI tumekusudia kufanya upasuaji mkubwa katika awamu hii lengo letu ni kuendelea kuokoa maisha ya wenzetu wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo,” alisema

 Dk. Disubhash Chandra wa Hospitali ya BLK alisema wataendelea kushirikiana na JKCI katika oparesheni mbalimbali za moyo.

Wakati huo huo, MOI nayo imewafanyia upasuaji wa kunyoosha uti wa mgongo watu sita.

  Daktari bingwa wa mgongo na upasuaji wa mgongo,  Nicephorus Rutabasibwa, alisema jana kuwa watu hao wamewekewa nati maalumu kunyoosha migongo yao.

“MOI tumefanya upasuaji huu kwa kushirikiana na madaktari wenzetu wa Hospitali ya BLK ya India.

“Lakini tunapokea pia watu wenye matatizo ya mgongo ambayo walipata kutokana na ajali mbalimbali kama ya gari, bodaboda na kuanguka kwa sababu  wengine wanaougua mgongo hukimbilia kwa waganga wa kienyeji.

“Nawasihi wawahi hospitalini kwa sababu matibabu yapo, waje tuwatibu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles