28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

WAFANYAKAZI WEZI U/NDEGE KUFUKUZWA KAZI


NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Richard Mayongela, amesema mamlaka hiyo itawachukulia hatua watumishi wezi ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi, kwani ina uvumilifu sifuri kwa wenye tabia hiyo.

Mayongela alitoa tamko hilo Dar es Salaam jana Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu abiria anayedai kuibiwa pochi yake Septemba 8, mwaka huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akisafiri na Ndege ya Emirate kuelekea ughaibuni.

“Kiwango cha kumvumilia mtumishi mwizi ni sifuri, tunawafukuza wengi na sasa tumeanza utaratibu wa upekuzi wa kiusalama kwa kila mtumishi na wale wenye ajira mpya ili kujua historia zao,” alisema.

Alishauri abiria anapokutana na kadhia yoyote ikiwemo ya kuibiwa atoe taarifa kwa maofisa waliopo kwa wakati huo na kuripoti polisi ili jalada lifunguliwe na suala lake lifanyiwe uchunguzi kwa lengo la kupata haki yake.

“Kwa Watanzania, hii ni nchi yetu mtu anaposambaza taarifa kwenye mitandao ya kijamii ukipaka matope taasisi yoyote ya serikali na huduma tunazotoa unaharibu taswira ya ya nchi yako. Kufanya kitendo hicho unakuwa umechafua nchi na kutenda makosa ya jinai,”alisema.

Akizungumza na MTANZANIA, Awatif Akrabi anayedai kuibiwa pochi yake Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, wakati akisafiri kuelekea Ughaibuni, alisema alipolalamika alisaidiwa kupata maelekezo kutoka kwa maofisa waliokuwepo.

Alisema mlalamikaji huyo alielekezwa kufungua jalada la uchunguzi lakini alikataa na alipotaka kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi kumbukumbu akaangalie aliyemuibia walimkatalia kwa sababu sio utaratibu.

Alisema uchunguzi ulifanyika na bado polisi wanaendelea kuchunguza tukio hilo na kwamba aliwaasa Watanzania kufuata utaratibu huo kwani sio utaratibu kumruhusu mtu asiyehusika kuingia katika chumba cha kuhifadhia kumbukumbu.

Ndugu wa abiria huyo Wael Akrabi, alisema ni kweli walionyeshwa mkanda huo lakini hawezi kutetea upande mmoja, dada yake aliibiwa kwenye ukaguzi.

Alisema alifika hapo jana kwa ajili ya kufuatilia pochi la dada yake na taarifa aliyopewa ili amfikishie dada yake aombe radhi ilimfikia na alipojaribu kumtafuta ndugu yake hakuweza kumpata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles