24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyakazi watano Azam Media wafariki dunia, watatu wajeruhiwa ajalini

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Watu saba wakiwamo wafanyakazi watano Uongozi wa Azam Media Limited, wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea kati ya Shelui na Igunga.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Julai 8 asubuhi, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na lori wakati wafanyakazi hao wakiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya kwenda kuonesha matangazo ya moja kwa moja ya uzinduzi wa Hifadhi ya Burigi kesho Jumanne Julai 9.

Uongozi wa Azam Media umethibitisha wafanyakazi waliofariki kuwa ni Salim Mhando, Florence Ndibalema, Said Haji, Sylvanus Kasongo, Charles Wandwi na dereva na utingo wake ambao majina yao hayajafahamika.

Wengine wawili waliojeruhiwa na wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ni Mohamed Mwinshehe, Mohamed Mainde na Artus Masawe ambaye hali yake inadaiwa kuwa nzuri kiasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles