31.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyakazi Tigo walioibia wateja wakiri, warejesha fedha kwa DPP

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

WAFANYAKAZI watatu wa Kampuni ya mawasiliano ya Tigo na wafanyabiashara wawili, wamekiri makosa ya kujipatia zaidi ya Sh milioni 20 kwa ulaghai kutoka kwa wateja na wamerejesha fedha hizo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Washtakiwa hao walikiri makosa na kutiwa hatiani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Kabla ya kupewa adhabu, Wakili wa Serikali Mkuu, Awamu Mbagwa, alidai washtakiwa waliingia makubaliano na DPP hivyo hawatarajii wapewe adhabu kubwa.

Washtakiwa walijitetea kwa kudai kwamba ni wakosaji wa mara ya kwanza, hivyo aliomba mahakama iwahurumie na kuwapa adhabu ndogo.

Baada ya hoja hizo, mahakama iliwahukumu kifungo cha nje miezi sita, huku sare za jeshi, simu 13 na line zake walizokutwa nazo zinataifishwa na kuwa mali ya Serikali na wamesharejesha fedha zote Sh milioni 20.3.

Wafanyakazi hao wa Tigo kutoka Mlimani City na Makao Makuu ya kampuni hiyo ni Kokubelwa Karashani, Godfrey Magoye na Khalfan Milao ambao ni watoa huduma kwa wateja.

Wafanyabiashara ni Mohamed Abdallah na Moses Kilosa ambao walikuwa hawana kazi, waliotajwa kuwa marafiki wa wafanyakazi wa Tigo, kazi yao kutapeli.

Hakimu Rwizile alipokuwa akitafakari adhabu dhidi ya washtakiwa hao, alisema makosa waliyofanya si mepesi, na kwa mujibu wa sheria anayepatikana na hatia katika makosa hayo, atatumikia kifungo, hivyo lazima adhabu kali itolewe ili kupunguza makosa ya mtandao.

Awali kabla ya kutiwa hatiani, Wakili wa Serikali Mkuu, Awamu Mbagwa alisoma hati mpya ya mashtaka na mashtaka matano likiwemo la kutakatisha fedha yaliondolewa.

Mbagwa aliwasomea shtaka moja la kujipatia Sh 20,378,627 kutoka kwa wateja mbalimbali wa Tigo kwa ulaghai.

Walikiri makosa hayo, wakasomewa maelezo ya awali ambapo ilidaiwa fedha hizo za wateja walitapeli Dar es Salaam na Arusha.

Jamhuri wametoa vielelezo mbalimbali zikiwemo sare za jeshi, simu za mkononi 13 alizokuwa nazo mshtakiwa wa kwanza na wa pili ambao hawakuwa na kazi, walikuwa mtaani wakitapeli.

Mashtaka yaliyoondolewa yalikuwa sita, likiwemo la kutakatisha Sh milioni 20.3 na mengine ni kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka katika akaunti za wateja, kuingilia mifumo ya kifedha ya Tigo Pesa bila kibali na kupatikana na mavazi ya JWTZ.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles