28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyakazi Tanzanite One walipwa milioni 40

Mwandishi Wetu – Arusha

Licha ya kusimamisha uzalishaji madini ya vito ya Tanzanite, Kampuni ya uchimbaji ya Tanzanite One imeanza kulipa madeni ya mishahara kwa wafanyakazi wake.

Hatua hiyo imechukuliwa na uongozi wa kampuni ili kuwapunguzia ugumu wa maisha wafanyakazi wake kutokana na kusimamisha uchimbaji kwa miaka miwili.

Baadhi ya wafanyakazi wameiambia Mtanzania Digital kwamba licha ya kupokea mshahara wa mwezi mmoja wanaamini utawasaidia kupunguza ukali wa maisha unaowakabili.

“Tumesimama uzalishaji kwa miaka miwili, tumelipwa mshahara wa mwezi mmoja si sawa na kukosa kabisa tunaendelea kusiliza viongozi wetu,” amesema mfanyakazi Elisante Msuya.

Kampuni hiyo ilikuwa na wafanyakazi 700 baada ya kusitisha uchimbaji ilibakiza wafanyakazi takribani 70 waliobakia kazini kwa shughuli za ulinzi wa migodi na masuala mengine.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya ulinzi Tanzanite One, Abubakar Lomba  amesema malipo hayo yamerejesha ari ya wafanyakazi hao walioanza kukata tamaa.

Naye Katibu wa kampuni hiyo, Kisaka Mzava alikiri Tanzanite One kulipa Sh milioni 40 za mshahara wa Desemba mwaka jana kwa wafanyakazi waliopo kazini.

“Kila tutakapopata fedha kutoka vyanzo vingine tutajitahidi kuzielekeza kwenye mishahara ya wafanyakazi wetu,” amesema Mzava.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles