24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyakazi 10 OBC wapandishwa kizimbani

Mwandishi Wetu, Arusha

Raia 10 wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), wamepandishwa kizimbani jijini hapa na wakidaiwa kufanya kazi nchini kinyume cha sheria.

Watuhumiwa hao walikuwa wakifanya kazi kitalu cha uwindaji wa kitalii kinachomilikwa na Kampuni ya Ortelo Business Corporation (OBC), iliyopo Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Niku Mwakatobe ilidaiwa Novemba mwaka jana hadi Januari mwaka huu raia hao walitenda kosa hilo kinyume cha sheria ajira za wageni.

Mwendesha Mashitaka kutoka Idara ya Kazi mkoani Arusha Immanuel Mweta aliwataja watuhumiwa wanaodaiwa kutenda kosa hilo kuwa ni Mohammad Tayyab, Ali Bakhash, Abdulrahman Mohammed, Martin Crasta.

Wengine ni Darwesh Jumma, Riaz Aziz Khan, Imtiaz Feyaz, Arshad Muhammad, Hamza Sharif na Zulfiqar Ali ambapo  kwa pamoja watu hao wanadaiwa kutokuwa na vibali vya kufanya kazi ndani ya nchi.

Kwa mujibu wa mawakili wanaowawakilisha mahakamani hapo Wakili Daudi Haraka na Godluck Peter, watuhumiwa hao waliokuwa hawajui lugha ya Kiingereza wala Kiswahili walipinga tuhuma zinazowakabili.

Washtakiwa hao walitolewa kwa dhamana kwa masharti kuwa na wadhamini wawili watakaokuwa na barua za utambulisho na mali kauli yenye thamani ya Sh milioni tano.

Watuhumiwa wote walikidhi masharti ya yaliyotolewa na mahakama hiyo ambapo watatakiwa kufika mahakamani hapo Februari 22, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles