22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Wafanyabiashara watakiwa kujisajili kupata TIN bure

Mwandishi wetu -Pwani

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imewataka wafanyabiashara kujisajili na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kuwa inatolewa bure bila malipo yoyote.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, alisema TRA inawataka wafanyabiashara wote ambao hawajajisajili kufika ofisi za TRA katika wilaya na mikoa ili waweze kusajiliwa waweze kufanya biashara zao kwa uhuru na kulipakodi stahiki.

“Tunafanya wiki ya huduma na elimu kwa lengo la kusogeza huduma karibu na walipakodi na kuwatatulia changamoto zao zinazohusu ulipaji kodi,” alisema Kayombo.

 Baadhi ya wananchi, wafanyabiashara waliofaidika na namba ya utambulisho wa mlipakodi waliipongeza TRA kuwafikia katika maeneo yao.

TRA inafanya wiki ya elimu kwa mlipakodi kwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara wote wakipita hadi madukani katika mikoa ya Morogoro na Pwani lengo ni kusogeza huduma karibu na walipakodi na kutatua changamoto zao zinazohusu ulipaji kodi.

TRA inafanya wiki ya huduma na elimu kwa mlipakodi katika mikoa ya Pwani na Morogoro kuanzia juzi hadi 17 kwa lengo la kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa wananchi ili kuongeza ulipaji kodi kwa hiari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles