23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara wataka waliotorosha madini wachukuliwe hatua

Eliya Mbonea, Arusha

Chama cha Wafanyabiashara wa madini Taifa (TAMIDA), kimetaka sheria ichukue mkondo wake dhidi ya waliohusika na utoroshwaji madini yenye kilo 31.159 kuhakikisha wanafungwa na kufanya kazi ngumu.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Sammy Mollel, alipokuwa akitoa tamko kuhusiana na jaribio hilo la kutorosha madini aina nane tofauti nje ya nchi.

Madini hayo yaliyotoroshwa yalikuwa ni Tsavorite, Tanzanite, Aquamarine, Ruby, Grissulate, Tourmaline, Spinel na Sapphire ambayo yalikamatwa hivi karibuni mpaka wa Namanga upande wa Tanzania yakiwa ndani ya basi tayari kuvushwa nchi ya Kenya kinyume cha sheria za Tanzania.

Mbali ya baadhi ya watuhumiwa kuendelea kushikiliwa na vyombo vya dola, Mollel katika tamko la TAMIDA ameiomba serikali kuhakikisha inausaka mtandao mzima na kuutia nguvuni.

“Waliohusika na jaribio hilo watiwe nguvuni, adhabu kali itolewe, walipe faini, kifungo na kazi ngumu iwe fundisho kwa wengine wasiokuwa waaminifu na wapinga maendeleo bila kujali uraia wao,” amesema Mollel.

Aidha amesema jaribio hilo lililenga kuhujumu uchumi wa nchi kwani tayari serikali imekwisha kuboresha na kuweka mazingira mazuri ya kuhamasisha wachimbaji kuuza madini yao katika masoko yaliyoanzishwa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles