29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Wafanyabiashara wampongeza JPM kuimulika TRA

Na TUNU NASSOR -DAR ES SALAAM 

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania, imeunga mkono kauli ya Rais Dk. John Magufuli kwa kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuangalia upya viwango vya ulipaji kodi kwa lengo la kuziba mianya ya ukwepaji kodi.

Kauli hiyo ya JWT imekuja siku chache baada ya Rais Magufuli kutoa agizo hilo wakati akiwaapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha atakayeshughulikia sera, Adolf Ndunguru na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Msafiri Mbibo, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa JWT, Stephen Chamle, alisema wanaunga mkono kwa dhati kwa kuwa wafanyabiashara wa kati na wa dogo ndio wahanga mifumo ya kodi nchini.

Alisema kwa sasa ilivyo ni kama adhabu kwa wafanyabiashara wachache ambao wameamua kuwa walipa kodi badala ya kuwalea na kuwasaidia wanabebeshwa mzigo wote.

“JWT tumekuwa tukitoa mapendekezo kadhaa kwenye mamlaka husika, ambapo mojawapo ni hili lililozaa agizo la rais, hivyo ni katika kumuunga mkono rais ambayo pia tumeshayatoa kwenye kikosi kazi cha Wizara ya Fedha na Mipango,” alisema Chamle.

Alisema katika mapendekezo ya wadau kwenye mabadiliko kwenye sheria za kodi  mwaka wa fedha 2019/ 2020 ikiwamo kuanzishwa kanda za kibiashara ambazo zitavutia nchi zinazozunguka mipaka yetu hasa zisizo na bandari.

“Hii itasaidia kuvutia kufanya biashara kubwa na Tanzania na tunapendekeza maeneo yatakayofaa ikiwemo Kariakoo, Mwanza, Tanga, Songwe, Mtwara, Dodoma pamoja Kigoma,” alisema Chamle.

Aliongeza kuwa kwa upande wa forodha, waliishauri Serikali itazame upya kuwapo kwa bei elekezi kwa bidhaa zote zinazoingia ndani ya nchi kama ilivyo kwenye magari.

“Pendekezo hili lilipotumika mwishoni mwa mwaka 2015 hadi mwanzoni mwa 2016, lilileta ufanisi mkubwa kwenye makusanyo na hatimaye kukawa na mlipuko wa kuvuka malengo kwa mara ya kwanza, lakini kwa bahati mbaya zikaondoshwa bila sababu ya msingi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,905FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles