25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

WAFANYABIASHARA WALIA NA TRA, UTITIRI WA TOZO

Na ELIZABETH HOMBO

Mara baada ya kumaliza kuzungumza, Rais Magufuli alitoa nafasi ya kwa wafanyabishara hao kutoa hoja na changamoto zinazokwaza biashara zao ambapo mfanyabiashara wa mafuta kutoka mkoani Mwanza, Agustino Makoye alisema  ukusanyaji wa tozo ya ushuru wa huduma mkoani humo ni wa vitisho kwani wahusika wamekuwa wakitumia silaha

Alisema pamoja na kufanya biashara halali na kutakiwa kulipia tozo hiyo ya asilimia 0.03 itokanayo na mauzo; “Wanakuja wanakuambia tangu mwaka 2015 hadi 2017 unadaiwa Sh milioni 200 na wewe una mtaji wa Sh  milioni 20,000 kwa hiyo Rais  nikuambie ukweli, wananchi hawa  wanachonganishwa na watumishi wasio waaminifu.

“Utakapoambiwa Sh milioni 200 utaambiwa ndani ya siku saba uzilete, utakapozunguka mlango wa nyuma utaambiwa leta Sh milioni 20 na ile ya kwanza haipo,”alisema Makoye.

Makoye pia alilalamikia utitiri wa tozo katika mafuta yatokayo nje ya nchi  ambayo alisema hulipiwa tozo zaidi ya 20.

Naye mfanyabiashara wa mafuta kutoka Singida, alisema amelazimika kufunga kiwanda chake Mkoani Arusha kwa sababu ya kodi nyingi.

“Hawa wakusanyaji wa kodi sifa yao kubwa imekuwa ni kufunga viwanda na hawatushauri tunafanyaje ili tusonge mbele.

“Mfano nalipa kodi 41, kila mmoja anataka apewe ushuru. Watu wengi hapa wameongelea ‘service levy’ sasa haya yote nilipie wapi. Hii ni changamoto kubwa ukiuliza manispaa wanakwambia lipa kila mahali.

“Ushuru wa mashudu tunachajiwa kutoka wizarani sijui wana nguvu gani na huko barabarani wanachaji tena na gari inakamatwa na ikilala ni fedha nyingi tena unachajiwa.

BUTI ZA JESHI 5,000

Ofisa Usalama wa Kiwanda cha bora, Sylivery Buyaga alisema licha ya kutengeneza buti nzuri za jeshi kwa miaka mitatu sasa lakini jeshi la Tanzania bado linaagiza viatu nje.

Alisema wamekuwa wakijitahidi kuzalisha viatu hivyo kwa ubora wa hali ya juu kwa kutumia mashine nzuri na wameajiri zaidi ya watu 400 lakini mwitikio wa kuungwa mkono na jeshi nchini ni hafifu.

“Nasema haya kwa masikitiko makubwa, hadi sasa tuna pea 5,000 zilizo stoo lakini sasa tumejaribu kujitanua kwenda nje ya nchi kutafuta masoko lakini wanataka waone kwanza kama Tanzania ambako ndiyo nyumbani tumefanya nini hakuna kilichofanyika.

“Nchi ya Rwanda na Uganda waliomba kiwanda hicho kipelekwe nchini kwao na majeshi yatakuwa yananunua kila mwaka lakini kutokana na uzalendo suala hilo lilishindikana.

“Uganda tulipewa na eneo, viongozi wangu.. na barua nyingi nimeandika lakini hakuna aliyejibu barua hizo, “ alilalamika.

Alisema kuhusu ubora wa ngozi, kutokana na mahitaji ya ngozi kutoka sehemu mbalimbali lakini wamekuwa wakiuziwa isiyokuwa na kiwango cha juu huku ile ya daraja la kwanza ikiuzwa katika nchi ya Kenya.

“Pia sekta hii ya ngozi ina matatizo makubwa sana kuanzia uchinjaji, ukusanyaji wa ngozi hadi kwa wale wanao process shida kubwa ninayoiona hapa ni sekta hii kuwa chini ya Wizara ya Viwanda na biashara wakati wataalamu wa ngozi waliosomea wako wizara ya mifugo, mimi nilikuwa naona sekta hii ingerudi kule kwa wataalamu waliosomea,”alisema.

RCO MORO ASIMAMISHWA

Kwa upande wake, mfanyabiashara kutoka Morogoro alisema wafanyakazi wa kiwanda cha tumbaku wamewekwa ndani bila kufunguliwa mashtaka.

Kutokana na hilo, Rais Magufuli alimsimamisha  Waziri wa Uwekezaji, Angella Kairuki kujibu hoja hiyo ambapo alisema  tayari aliwasiliana na  Wizara ya Mambo Ndani ya Nchi kwa ajili ya kuchukua hatua.

Majibu hayo yalionekana kutomridhisha Rais Magufuli ambaye kabla hajamsimamisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, alisema yeye mwenyewe alimsikia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumzia suala hilo lakini hakuona hatua iliyochukuliwa.

Akijibu hoja hiyo, Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani, alisema suala hilo wanalishughulikia na Rais Magufuli alipohoji aliyewaachia watu hao ni akina nani alisema ni Mkuu wa Upepelezi Mkoa wa Morogoro (RCO) na kutaka hapo hapo asimamishwe kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles