27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara walalamikia bei ya limao

 SARAPHINA SENARA (UOI)– DAR ES SALAAM

WAFANYABIASHARA katika masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam wamelalamikia kupanda kwa bei ya malimao ikiwa ni pamoja kuwa na uhitaji mkubwa hasa kwa watu wanaofanya biashara ya lishe katika huku ikiwachukua muda mrefu kuyapata, ukilinganisha na kipindi cha mwanzo ambapo ilikua rahisi kuyapata.

Wamesema wakati huu upatikanaji wa malimao umekua mgumu kwa sababu sio msimu wake huku wakidai kuwa hata wateja wao pia wamekua wakilalamikia bei kuwa juu kwani sasa limao moja linauzwa kwa bei ya Sh 500 tofauti na kipindi kilichopita ambapo limao moja walikua wanauza kwa Sh 100 na upatikanaji wake ukiwa rahisi kulinganisha na wakati huu.

Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti walisema wamekua wakiagiza malimao hayo toka mikoani kwani kuyapata katika Jiji la Dar es Salaam imekua changamoto na wengine ikiwalazimu kupiga simu mapema ili wateja wasiweze kukosa huduma hiyo pamoja na kupoteza sokola biashara hiyo ya malimao.

Mmoja ya wafanyabiashara wa limao katika Soko la Mabibo, Juma Shabani alisema wamekua wakiagiza malimao kutoka mikoani na pale ambapo yanakaribia kuisha imemlazimu kupiga simu mapema ili asiweze kupoteza wateja wake wanaohitaji malimao na baada ya siku mbili anaweza kuyapata.

“Nikiona yamebaki kidogo ninawapigia simu watu wa magari wanaoleta mizigo ili niyapate yasiishe kabisa maana siku hizi yamekua na shida kupatikana kwahiyo inakuwa rahisi kama nikipiga simu mapema alafu nisubiri waniletee ili nisije nikakosa kabisa malimao maana yamekua adimu,” alisema Shabani.

“Tunachelewa kupata mapema kwasababu hayapatikani sana hapa kwahiyo kama jana mimi nimepata nfio maana leo yapo ila nikiona tu yamebaki machache lazima nipige simu maana sijui hata wanachukulia mkoa gani ndio maana natoa taarifa mapema,” aliongeza.

 Mfanyabiashara katika Soko la Mabibo, Joyce Aloyce alisema yeye kwa sasa hauzi malimao tena kwa sababu hayapatikani kwa urahisi kama mwanzo na pia kwasababu wote wanafanya biashara ameamua kuendelea na biashara ya nyanya chungu huku akiwaachia wengine kuendelea na biashara ya malimao ila akidai kuendelea na biashara ya malimao wakati mwingine.

“Mimi hapa nilikua nauza lakini haya hapa sio ya kwangu kwa sababu bei imekua juu sana, kwahiyo inabidi tufanye biashara kwa kupokezana pamoja na kuwa huu sio msimu wa malimao kwahiyo imekua kazi sana kuyapata ndio maana na bei yake imekua kubwa kwasababu hayapatikani tena mpaka utakapofika msimu wake,” alisema Aloyce.

Mfanya biashara wa matunda na mbogamboga katika Soko la Tegeta kwa Ndevu, Husna Amiri alisema bei ya limao imekua juu sana kwa sababu pia hata matumizi ya watu yamekua makubwa akidai kuwa tangu kipindi cha ugonjwa wa Covid-19 watu wamekua wakinunua kwa wingi limao maana walikua wanatengeneza kwa kuchanganya na tangawizi kama dawa.

“Huu ndio sio msimu wa limao lakini wateja bado wanahitaji kununua kwa ajili ya matumizi yao na wengine wanashangaa sana ukiwaambia limao shilingo 500 kwa moja, wakati mwingine wanaondoka na baadae wanarudi baada ya kukuta haya hapa ni mazuri na bei ni moja kwa hiyo wanajikuta wananunua japo kwa kulalamika,” alisema Amiri.

Mmoja wa wateja katika Soko la Tegeta kwa Ndevu ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kupanda kwa bei ya limao gafla kumefanya watu wengi kushindwa kununua malimao na hivyo kushindwa kutumia kwenye chakula.

“Yaani nikisema ninunue ndimu ya unga inakua tofauti sana na limao yani ile inakua kali kulinganisha na limao ndio maana watu wengi ambao tunanunua limao kwa matumizi ya nyumbani tunapenda kununua limao ndio maana tunajitahidi tu kununua hata hayo mawili matatu kutokana na bei,” alisema.

 Matumizi ya limao yanategemeana na mtu au aina ya chakula lakini wakatyi wa kipindi cha ugonjwa wa korona watu wengi wamekua wakitumia limao kwaajili ya kutengenezea dawa yenye mchanganyiko wa tangawizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles