29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara wa Samaki Moshi wamuangukia Chongolo

Safina Sarwatt, Moshi

Wafanyabishara wa samaki waliondolewa katika soko la Manyema kwenda Pasua Manispaa ya Moshi wamemlilia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Daniel Chongolo wakitaka warejeshwe soko lao la awali.

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akizungumza kwenye mkutano huo.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Halmashauri ya Manispaa hiyo iliwahamisha wafanyabiashara hao kwenda soko la Pasua kata ya Bomambuzi kwa madai soko la Manyema halikuwa na miundombinu rafiki.

Wafanyabiashara hao wametoa kilio hicho Agosti 3, kwenye moja ya mikutano ya Katibu huyo Mkuu wa CCM ambaye anaendelea na ziara ya siku nne mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya wafanyabiashara hao, Ester Mariki na Salma Kiondo wamesema tangu wameondolewa katika soko hilo wameshindwa kufanya biashara zao kutokana na kutokuwa na wateja wa kutosha.

Kufuatia kilio hicho, Chongolo amemwagiza mkuu wa wilaya ya Moshi Abbas Kyada kutuma timu ya wataalamu kufanya ukaguzi na thamini eneo hilo kama linafaa kwa biashara na kuandaa mchoro.

“Mkuu wa wilaya wewe ni kamisaa wa CCM nakupa wiki moja nataka uniletee mchoro na thamini ya gharama zake ili wafanyabiashara hao wapate mahali pakufanyiabishara zao,” amesema Chongolo .

Mkuu wa Wilaya Moshi, Abas Kyada amesema halmashauri ya Manispaa ya Moshi ilitenga kiasi cha Sh milioni 250 kwa ajili ya ukarabati wa soko la Pasua.

Amefafanua zaidi kuwa halmashauri iliona soko la Manyema halikuwa na mazingira rafiki ya kibishara na kwamba lilihamishwa ili kinusuru maisha ya wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles