23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara Temeke watakiwa kutumia fursa ongezeko la mikopo midogo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wanachama wa Klabu ya Wafanyabiashara Wanaohudumiwa na Benki ya NMB, Wilaya ya Temeke (NMB Business Club), wametakiwa kutumia fursa zitokanazo na ongezeko la kiwango cha mikopo midogo ya kuanzia Sh 500,000 hadi milioni 75 na kushuka kwa riba zake kutoka asilimia 21 hadi asilimia 14, ili kujiimarisha kiuchumi.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard akizungumza na Wafanyabiashara Wanaohudumiwa na Benki hiyo, Wilaya ya Temeke (NMB Business Club) jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la wafanyabiashara hao lililoandaliwa na NMB kuwajengea uwezo.

Wito huo umetolewa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, wakati wa Kongamano lililoshirikisha wanachama zaidi ya 150 wa NMB Business Club wilayani Temeke, lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa PR Hotel, jijini Dar es Salaam, ambalo lilifunguliwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ezekiel Gutti.

Akizungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali hao, Donatus alibainisha kuwa, NMB ambayo ni benki kinara miongoni mwa mabenki zaidi ya 50 nchini, ina mtaji wa kutosha unaowapa wateja wao uhakika wa usalama wa fedha zao na usiri wa taarifa za0. Na hii ndio imechangia zaidi ongezeko kubwa la kiwango cha mikopo midogo, sambamba na kushuka kwa riba za mikopo hiyo.

“Kiwango cha mikopo midogo midogo kinachoanzia Sh 500,000 hadi Sh milioni 50, sasa kimepanda hadi kufikia Sh milioni 75, wito wetu kwenu ni endeleeni kutumia fursa hiyo muhimu ya mikopo, ambayo kwa wale wateja wanaochiupikia, riba imeshuka kutoka asilimia 21 ya awali na sasa kuwa asilimia 14. Huduma hizi zipo matawini, karibuni,

“Mnachotakiwa kutambua tu ni ukweli kwamba ninyi mko katika benki sahihi, kwa sababu NMB tunaongoza wateja zaidi ya Sh milioni 4, hii ina maana mnahudumiwa na benki inayoaminiwa zaidi nchini. Tunaongoza pia kwa faida, na hii lazima tuwashukuru ninyi, kwani kupitia ninyi ndo tumeongoza faida hadi Desemba 2021 ya Sh milioni 289.

Donatus aliwataka wanachama hao kuwa mabalozi wema wa NMB katika jamii inayowazunguka, ili kuongeza idadi ya wanufaika wa huduma mbalimbali, kama za bima, zikiwemo za vikundi vya kuanzia watu watano na kuendelea, ambazo zinatoa kinga na kutoa fidia kwa mwanachama na familia (mke/mume na watoto) anapofariki.

Kwa upande wake, Mtoa Mada Mkuu wa Kongamano, James Mwang’amba, aliwataka wafanyabiashara na wajasiriamali walioshiriki Kongamano hilo kuhakikisha wanakata ‘minyororo isiyoonekana’, ambayo imekuwa ikikwaza ustawi wa biashara na kuyumbisha ukuaji kibiashara na kiuchumi miongoni mwao.

Mwang’amba aliitaja ‘minyororo sita iyoonekana’ inayowakwamisha wengi wao kuwa ni pamoja na Kuamini kuwa mafanikio ni mchakato wa polepole, kuachana na dhana ya mtu kujiona ama kuamini hawezi, kuwaepuka ndugu, jamaa, marafiki na watu wa karibu wanaokatisha tama na kiwango kidogo cha uwezo wa kumiliki hisia hasi.

Minyororo mingine iliyotajwa na Mwang’amba katika Kongamano hilo lililowashirikisha pia wadau wa biashara wakiwamo Kikozi cha Zimamoto na Uokoaji, Kampuni za Bima ni tabia ya mtu kujaribu kumsaidia ama kumuokoa kila mtu anayezunguka na mwisho ni kukosa mfumo sahihi wa kiutendaji – ikiwemo uagizaji, uratibu, usimamizi.

Awali akifungua Kongamano hilo, Mwenyekiti wa NMB Business Club Wilaya ya Temeke, Ezekiel Gutti, aliwataka wanachama wake kuyatumia vema mafunzo yatakayo tolewa, ili kuharakisha ustawi wa biashara na kuimarika kiuchumi, pamoja na kuyaorodhesha mapendekezo yao kwa NMB ili yafanyiwe kazi na uongozi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles