26.5 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Wafanyabiashara msiwakimbie TRA

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wafanyabiashara Mkoa wa Dar es salaam wameshauriwa kutowakimbia maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanapowatembelea katika maeneo yao ya biashara bali watoe ushirikiano ili waweze kufaidi elimu na ushauri unaotolewa na maofisa hao.

Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wafanyabiashara wa Tabata Segerea jijini Dar es Salaam ambao walipata fursa ya kupatiwa elimu wakati wa zoezi la kuelimisha wafanyabiashara katika maeneo yao ya kazi huku wafanyabiashara wengine wakifunga maduka yao.

“Nimepata mafunzo mazuri baada ya kuwapatia maelezo ya biashara yangu na mapungufu niliyonayo,wamenielimisha vizuri na kunishauri mambo mazuri kuhusu biashara yangu, mfanyabiashara hana sababu ya kufunga duka au kusingizia kwamba mwenye duka hayupo kwani kufanya hivyo ni kupoteza nafasi ya kuelimishwa,” alisema Jamila Mgeni mfanyabiashara wa nguo Tabata Segerea.

Jamila amesema endapo mfanyabiashara ana changamoto katika makadirio ya kodi ni vema akakubali kutembelewa na maofisa wa TRA ili wamsaidie na kumuelekeza nini cha kufanya.

Katika hatua nyingine mfanyabiashara huyo aliwasihi wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati ili shughuli ambazo zinafanywa na serikali za kijamii na kiuchumi ziweze kutekelezwa kwa ukamilifu.

Naye Babin Mohammed mfanyabishara wa nguo za mtumba amesema wanaowakimbia maofisa wa TRA inawezekana kuna makosa wanayoyafanya au wana mapungufu hivyo ni vema wakubali kuwasikiliza ili waweze kusaidiwa kwa kuelimishwa na kupatiwa ushauri wa kutatua changamoto zinazowakabili.

Akizungumzia zoezi la kuwatembelea wafanyabiashara maeneo yao ya biashara, Afisa Msimamizi wa Kodi, Lameck Ndinda amesikitishwa na wafanyabiashara ambao wanafunga maduka yao na kuwashauri kutoa ushirikiano ili lengo la zoezi hilo liweze kufanikiwa.


“Lengo la zoezi hili ni kuwaelimisha wafanyabiashara, kufahamu changamoto zinazowakabili, na kupata maoni yao na ushauri kuhusu huduma zinazotolewa na TRA”, amesema Ndinda.

mesema kuwa wafanyabiashara hawana sababu ya kuwakimbia maofisa wa TRA kwani wanapowatembelea wanawapatia ya fursa kuuliza maswali na kuwapatia utaratibu wa kusajili bishara zao wale ambao hawajasajiliwa
amesema kwamba zoezi hili ni endelevu na kwa sasa linaendelea katika Mkoa wa Dar es salaam na baadae katika mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya na Tanga.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles