Wafanyabiashara dawa za kulevya wapewa onyo

0
606

Mohammed Ulongo

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya imetoa rai kwa wote wanao jihusisha na biashara ya dawa za kulevya waache na wajihusishe na shughuli zilizokuwa za halali kwani mkono wa Sheria utawafikia popote walipo pindi wakiwa wanajihusisha na shughuli hizo .

Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu Kamishna Jenerali James Kaji alipokutana na waandishi habari kuzungumzia juu ya kukamata dawa za kulevya aina ya Heroin zaidi ya kilo moja na nusu katika mikoa ya Dar es salaam na Mwanza .

Aidha Kamishna ameongezea kuwa wamekamata zaidi ya kilo 214 za vifurushi vya dawa za kulevya aina ya mirungi zilizokuwa zikisafirishwa kwa njia ya posta kutoka Arusha kwenda nchini Uingereza .

Ukamataji huo wa vifurushi vya dawa za kulevya aina ya mirungi kwa njia ya posta ni muendelezo wa ukamataji uliofanywa na Mamlaka kwa kushirikiana na Shirika la Posta.

Wizara ya kilimo na mifugo na wizara ya Maliasili na utalii nchini ambapo zaidi ya kilo 300 za dawa za kulevya iliyokuwa ikingizwa nchini kutoka Ethiopia na kusafirishwa kwenda nchi za ulaya hasa Uingereza kwa njia ya Posta, kwa kutumia majina bandia ya Mlonge, Moringa tea, dawa, majani ya mboga, tea leaves na Moringa leaves .

Hata hivyo mamlaka imesema kuwa inamshikilia aliyekuwa Afisa Usalama wa Shirika la Posta Tanzania, George Arsein even kuhusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya kwa njia ya posta.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here